Viongozi wa Kanisa la Moraviani Parishi ya Sabasaba mkoani Singida wakiwa nje ya kanisa baada ya kumaliza ibada ambayo walimuombea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wote na chama hicho kwa kutimiza miaka 46 tangu kianzishe mwaka 1977. Kutoka kushoto ni Mzee wa kanisa hilo, Obed Mwalwiba na Muhubiri katika ibada hiyo, Israel Mwaisela. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

KANISA la Moravian Parishi ya Sabasaba mkoani Singida wamemuombea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  na wanachama wote wa chama hicho kwa kushereheka maadhimisho ya miaka 46 tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1977 ambapo kilele chake ni leo na mkoani Singida sherehe hizo zinafanyika Kata ya Minyughe wilayani Ikungi na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa,  Martha Mlata na Katibu Mwenezi Ahmed Kaburu.

Pongezi hizo zilitolewa katika ibada iliyofanyika leo Februari 5, 2023 ambapo muhubiri Israel Mwaisela alisema chini ya chama hicho na Serikali yake nchi imekuwa na amani na utulivu na watu wamekuwa wakipata fursa ya kuabudu tofauti na nchi nyingine ambazo zimepoteza amani kwa sababu mbalimbali ikiwemo vita.

"Wakristo wa Moravian tuna kila sababu ya kumuombea Rais wetu Mama Samia Suluhu , na viongozi wote na chama kilichopo madarakani ambacho leo kinatimiza miaka 46 tangu kuanzishwa kwake kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuifanya nchi yetu kuwa na amani na utulivu" alisema Mwaisela.

Akihubiri katika ibada hiyo Mwaisela alielezea umuhimu wa utoaji wa misaada kwa watu wenye uhitaji na wengine na kusema unapomsaidia mtu ndipo nuru yako inapoonekana mbele za sMungu.

"Neno la Mungu linasema asiye na nguo tumvike, na kuwa hayo ni maneno yanayoelekeza kutoka katika biblia kitabu cha injili na kuwa tunaishi na watu wasio na uwezo kabisa lakini wanashindwa kusaidiwa licha ya baadhi yetu kuwa na uwezo huo" alisema Mwaisela.

Mwaisela alisema kutoa ni moyo na wala sio fedha kwani kuna baadhi ya watu wanasema wataanza kusaidia baada ya kupata mafanikio jambo ambalo sio sahihi ambapo alihimiza watu kutosubiri wapate mafanikio ambayo hawajui watayapata lini ndipo waanze kusaidia badala yake waanze kutenda mema sasa na Mungu atawabariki.

"Anzeni kuwasaidia watu kwa kutoa kwa kile kidogo mlichonacho msisubiri mpaka kiwe kikubwa, ndipo moyo wa kutoa utajengeka ndani yako na hata utakapopata mafanikio utatoa vingi kwani ndani ya moyo wako hautakuwa na choyo tena" alisema Mwaisela.

Aidha Mwaisela alisema ukristo si kuhudhuria ibadani tu bali ni kumcha Mungu na kuacha maovu yote na kutenda mema ambapo alitolea mfano sawa na chumvi ilyoharibika itiwe nini hadi ikolee.

Alisema mkristo ambaye anakwenda kanisa kusali tu na baadae kuendelea na mambo yake ya kutenda dhambi huyo ni sawa na chumvi iliyoharibika hivyo aliwataka wakristo kubadilika na kuwa watenda mema mbele za Mungu.

Mzee wa kanisa hilo Obed Mwalwiba  alitumia nafasi hiyo kuwaomba waumini na wadau wengine mbalimbali kuendelea kuchangia ununuzi wa kiwanja cha kujenga kanisa hilo Parishi ya Sabasaba kwani hivi sasa wanasali kwa kutumia banda walilolijenga kwa miti na kuezeka kwa bati.

Aliomba kwa mtu yeyote atakayekuwa tayari anaweza kutoa kiasi chochote alichonacho kupitia Akaunti namba  50810046663 Benki ya NMB Kanisa la Moravian Sabasaba au wawasiliane na Mchungaji wa Kanisa hilo kwa namba 0758148508 kwani kutoa ni moyo wala sio utajiri na lengo ni kupata Sh. Milioni 10.

Muhubiri katika ibada hiyo, Israel Mwaisela akihubiri neno la Mungu.
Muumini wa Kanisa hilo, Jemina Kalinga akisoma matangazo.
Mwenyekiti wa Wanawake wa kanisa hilo, Agnes Mwaihojo akizungumza katika ibada hiyo.
Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ibada ikindelea.
Ibada ikiendelea.
Taswira ya ibada hiyo.
Waumini wakiwa nj baada ya ibada hiyo.
Nyimbo zikimbwa baada ya ibada hiyo.

Muonekano wa kania hilo.

Mmoja wa watoto wa kanisa hilo akionesha tabasamu baada ya ibada hiyo

Waumini wa kanisa hilo akiwa katika picha ya pamoja. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: