Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko, akiongozana na  viongozi wa Sekretarieti ya mkoa wakati  walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida  inayojengwa katika Kata ya Solya wilayani Manyoni.

Na Thobias Mwanakatwe, Singida 

MRADI wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida inayojengwa Kata Solya wilayani Manyoni mkoani Singida ambayo serikali ilishatoa Sh.Bilioni 3 awamu ya kwanza ujenzi wake umeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya mfumo wa malipo.

Kukwama kwa ujenzi huo kumebainika  baada ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko, alipotembelea kukagua mradi huo  akiwa ameambatana na sekretarieti ya mkoa na kukuta asilimia kubwa ya mafundi hawaendelei na kazi ya ujenzi.

Mwaluko amesema anashangaa kukwama kuendelea kwa ujenzi wa shule hiyo wakati fedha zipo na kwamba 'alijikomiti' kwenye kikao cha Kamati ya Bunge kwamba ujenzi utakamilika Disemba 2022 ili wanafunzi waanze masomo katika shule hiyo Januari 2023.

Naye kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Manyoni, Andrew Coromany, amesema ujenzi wa shule hiyo umekwama kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya mfumo wa malipo ambao umekuwepo tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Alipoulizwa kama je inawezekana mafundi hawajalipwa labda pesa zimekwisha, alisema fedha zipo na kwamba kati ya Sh.bilioni 3 zilizoletwa na serikali awamu ya kwanza zilizobaki hadi sasa ni Sh.bilioni 1.490.

Majadiliano yakifanyika wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa mradi huo.

Muonekano wa baadhi ya majengo ya shule hiyo ambayo ujenzi wake unaendelea. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: