Na, Imma Msumba ; Karatu

Sekta ya maji nchini imeendelea kuimarika kupitia utekelezaji wa miradi inayotoa huduma kwa wananchi.Jukumu hili linasimamiwa na Wizara ya Maji kuhakikisha rasilimali za maji zinatunzwa na kulindwa ili miradi inayojengwa iweze kukidhi maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Nchini Tanzania serikali kwa kushirikiana na wadau imepiga hatua katika kuboresha sekta ya Maji kuhakikisha watanzania popote pale walipo wanapata huduma ya maji.

Viongozi wameendelea  kufanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji zenye kutosheleza katika maeneo ya Vijijini na Mijini. Waziri wa Maji Juma Aweso  aliamua kuiondoa miradi ya maji kichefuchefu na kumtua ndoo mwanamke.

Juhudi hizi za rekiali, zimefanya kuwe na ongezeko la upatikanaji wa huduma za maji kwa wananchi wa maeneo mbalimbali hapa nchini na hii ni kutokana na Serikali kuwekeza katika miradi ya maji mikubwa na midogo.

Licha ya jitihada hizo za Serikali hali bado ni tete katika Wilaya ya Karatu iliyopo Mkoani Arusha ambapo wananchi wa wilaya hiyo  wanakabiliwa na adha kubwa ya upatikanaji wa maji na kupelekea wananchi hao kuamka  alfajiri huku wakihofia maisha yao kwakua nyakati kama hizo pana kua na giza wanyama kama vile fisi.

Akizungumza kwa uchungu mmoja wakazi wa karatu Recho Abeli alidai kuwa anapata wakati mgumu sana kutafuta maji muda huo wa alfajiri kutokana na majukumu ya familia na kulazimika kuchelewa kufanya shughuli za kuingizia kipato familia yake 

"Tunaishi kwa shida sana hapa  kwa sababu hakuna maji tunalazimika kwenda kuchota maji kuamka nyakati za alfajir binafsi lazima niamke ili niwahi foleni kwasababu nina wanafunzi wanahitaji kwenda shule kukipambazuka na wanahitaji kupata kifungua kinywa kadhalika nachelewa kufanya shughuli za  kuniingizia kipato, tukiwa njiani kwenda kutafuta maji tunahofia ulinzi wetu kwasababu tunahatarisha maisha yetu kutokana na nyakati tunazoamkia kutafuta maji tunaweza kukutana na wanyama au hata majambazi"

Akizungumza hali hiyo John Jacob ambaye ni mkulima na mkazi wa kitongoji cha Ayalabe amesema "Niiombe serikali kuangalia namna gani bora kwetu kupatiwa huduma za maji wakati wote ili tuwe na muda wa kufanya shughuli zetu za kutuingizia kipato kwasababu muda mwingi tunautumia kutafuta maji na tunachelewa kwenda kwenye biashara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Maji Juma Aweso wanafanya jitihada za kumtua mama ndoo kichwani kwa kupeleka miradi ya maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini lakini baadhi ya viongozi katika Serikali yake wanashindwa kuwasaidia wananchi.  Serikali kupitia Wizara ya maji imeendelea na kuzidi  kujimarisha  na kujipanga kimkakati kwa kufanya mageuzi Katika sekta ya maji Vijijini kwa kuanzishwa kwa  mfumo wa Maji wa malipo kabla ya matumizi (Prepared meter) ambapo mwananchi atapewa kadi na kuweka pesa kwenye kadi hiyo kabla ya kuchota Maji na kuweka kiasi cha pesa ambayo anataka atumie katika kuchotea Maji ili kuona mfumo huo unavyoleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi kupata maji kwa urahisi kwa masaa 24.

Mfumo huo umefanyiwa majaribio katika maeneo mbalimbali nchini mpaka sasa bado upo katika hatua za majaribio kwa kusaidia wananchi kupata maji wakati wowote masaa 24 bila kuwepo kwa msimamizi hapo kituoni na fedha zote zinakusanywa katika mfumo Maalumu na baadae kuwarejeshea Jumuiya ya Chombo kinachosimamia mradi huo kwaajili ya matumizi mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mji Mdogo wa Karatu (KARUWASA) Stephen James amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa maji kwa wananchi wake Wizara ya maji imeahidi kutoa mita elfu moja na tisini elfu (1,090) ambazo zinatarajiwa kuwasili muda wowote huku zaidi ya watu 160 wakijiandikisha na idadi kuongezeka kila siku kwa kutambua umuhimu wa maji.

“Tunasubiria vifaa ili kuwasaidia wananchi wetu wapate huduma nzuri za Maji kwa kufungiwa maji bila gharama yoyote na baadae kulipa kidogo kidogo kupitia billi ya kila mwisho wa mwezi na mpango huu unaendelea tunasubiria fedha tununue Mabomba yakutosha, na wizara imetuahidi mita elfu 1,090  lakini tunasubiri pia kupata vifaa vingine na zitakapotosheleza tutawatangazia wananchi ambao wanaendelea kujiandikisha na idadi inaongezeka kila siku. ”Alisema

James aliongezea kwa kusema mpango  wa malipo yabmaji kabla ya matumizi tumeshaanza nao na ni endelevu ambapo jumla ya vituo 10 vimeanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi wa Karatu mjini upande wa Tloma na  Gongali na wananchi kujipatia maji kwa kujihudumia wenyewe na mara kadi inapoisha hela kuongeza hela na kuendelea kutumia .Share To:

Post A Comment: