Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye ( Mb ) amesema serikali iko mbioni kutafuta namna ya kumuwezesha mtanzania wa kawaida kumudu gharama ya kununua simu janja.


Amebainisha hayo wakati akizindua mnara wa simu katika Kijiji cha Kinenulo kata ya Imalinyi mkoani Njombe.

Nape amesema hivi sasa wanafanya mazungumzo na makampuni ya simu . " Na Mimi kwa sababu naipenda kazi yangu nimeshaanza kuangaika tumebanana na makampuni ya simu tunatafuta utaratibu ambao makampuni ya simu na watoa huduma wengine wataleta simu walau iwe ni kwa mkopo mtu alipe taratibu lakini aipate huduma aanze kutumia "

Ameongeza kuwa "Maana yake mtu wa kawaida kuchukua laki tatu ukaenda kununua simu kidogo ngumu lakini tukimwambia weka elfu 30,000 upewe simu ya laki tatu alafu utakua unakatwa kidogo kidogo hata kama ni kwa mwaka mzima , huduma unapata , umepata kwa bei ndogo na maisha yanaendelea maagizo hayo ameyatoa Rais Samia "

Hata hivyo Nnauye alisema kuwa malengo ya serikali ni kuhakikisha kila mtanzania kokote alipo anaunganishwa na huduma ya mawasiliano .

"Dunia ya leo mawasiliano ni kila kitu , ukizungumza elimu , ukizungumza afya , ukizugumza biashara,ukizungumza huduma za kifedha yote haya ukiwa na mnara hivi mambo yanakwenda sawasawa " alisema Nnauye.

Afisa mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasilino kwa wote ( UCSAF ) Justina Mashiba,amesema wanajukumu la kupeleka huduma za mawasiliano vijijini na tayari wamejenga minara 1,087.

"Mkoa wa Njombe tunamiradi 32 , minara 32 katika hiyo minara 30 imekamilika na miwili ipo katika hatua mbalimbali utekelezaji na ruzuku iliyotolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote ni bilioni 4.8 ndo imetumika kwa ajili ya kupeleka kama ruzuku kwenye miundombinu ya mawasilino " alisema Mashiba





Share To:

Post A Comment: