Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete , ameanza ziara Jimboni kwake .


Katika ziara hiyo amekagua ujenzi wa madarasa 13 kata ya Msata ambapo Serikali ya Rais Samia imetoa milioni 280 kujenga madarasa hayo.

Vilevile, hasa kwa kuzingatia kipindi hiki cha kuelekea kufunguliwa kwa shule, Ridhiwani amegawa vifaa vya masomo kama madaftari, peni kwa wanafunzi ili waweze kutumia mashuleni.

"Serikali imeendelea kuleta fedha za maendeleo katika halmashauri yetu ya Chalinze, Huduma za afya, elimu, miundombinu ya barabara na kazi Inaendelea Chalinze." alifafanua Ridhiwani Kikwete...
Share To:

Post A Comment: