Mwenyekiti wa Halmashauri yaWilaya ya Mkalama James Mkwega akifungua kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la  kupitia na kujadili mapendekezo ya bajeti kwa Mwaka wa  fedha 2023/2024 kilichoketi mwishoni mwa wiki na kupitisha bajeti ya zaidi ya Sh. Bilioni 27.

Na Dotto Mwaibale, Mkalama

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mkalama, James Mkwega amewataka watumishi kufanya kazi kwa kushindana kila idara ili kuiletea maendeleo halmashauri hiyo na kuwaondoa hofu kuwa hakuna atakayefukuzwa kazi kama wanajituma kufanya kazi kwa bidii.

Mkwega ameyasema hayo wakati akifungua kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la  kupitia na kujadili mapendekezo ya bajeti ya kwa Mwaka wa  fedha 2023/2024 ambacho kilipitisha bajeti ya zaidi ya Sh. Bilioni 27.

“Watendaji fanyeni kazi kwa ‘kurelax’ hatuna mpango wa kumchukia mtumishi wala kumfukuza ila atakayependa kujifukuzisha mwenyewe tunamruhusu,” alisema Mkwega.

Alisema watumishi wanapofanya kazi na kuleta matokeo chanya ya maendeleo kwa wananchi wanatengeneza historia ambayo hataikitokea amekufa kuna alama ambayo ataiacha ambayo itazungumzwa na walio hai.

“Hapa mnajaziliza historia ili hata mtakapoondoka duniani kunajambo zuri litazungumzwa juu yenu, niwaombe na kuwatia nguvu watumishi jitumeni na endeleeni kufanya kazi kwa kushindana kwa kila idara.

Alisema katika utendaji wa kazi hakuna kitu kinacholeta mgawanyiko kama tafsiri ya ulaji,hivyo nawaomba kwenye ofisi zenu muepukane na jambo hilo.

Aidha, alisema katika mwaka huu wa fedha halmashauri inampango wa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuwaomba watumishi kushirikiana idara zote ili kufikia malengo ya kukusanya na kutumia zaidi ya Sh.Bilioni 27.

Mkwega alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo na timu yake kwa kuandaa bajeti nzuri inayozingatia vipaumbele na mahitaji ambayo ina kwenda kuleta mahitaji ya maendeleo ya wananchi.

Awali akisoma Rasimu ya Mpango wa bajeti, Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Daniel Tesha alisema nguvu kubwa wameielekeza katika ukusanyaji wa mapato ambapo wanategemea kuongeza ukusanyaji wa mapato huru ya ndani kutoka Sh. Bilioni 1.287 hadi Sh. Bilioni 1.333 ambazo kati hizo Sh. Milioni 302. 7 zitatumika kwa shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Sh.Bilioni 1.zitakuwa kwa ajili ya shughuli za uendeshaji.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Said Kalima alisema  atahakikisha bajeti hiyo inakwenda kufanya kazi kwa malengo yaliyokusudiwa.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bosco Samwel  akizungumza kwenye kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Said Kilima akizungumza.
Kikao kikiendelea.
Taswira ya kikao hicho.
Maswali yakiulizwa kwenye kikao hicho
Kikao kikiendelea.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkalama, Daniel Tesha akizungumza.
Michango mbalimbali ikitolewa kwenye kikao hicho.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Mkalama akizungumza.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Mkalama, Yasini Mohamed akitamburisha kwa madiwani  mpango mpya wa Takukuru Rafiki.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: