Mwenyekiti wa Kijiji cha Msomera wilayani Handeni   Martin Paraketi akizungumza katika kikao cha pamoja na wananchi  na mkuu wa mkoa wa Tanga Omoari Mgumba wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi , janury 23, 2023.


Mganga mkuu wa wilaya ya Handeni vijijini Kanansia Shoo akimwelekeza jambo mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati alipotembelea na kukagua mradi wa kituo hicho cha afya Msomera kinachoendelea kujengwa ambacho kimegharimu shilingi Million 500.


Na Denis Chambi, Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba amewataka wananchi waliovamia katika maeneo ya Poli tengefu lililokuwa limetengwa na serikali wilayani Handeni kwaajili ya malisho na kuanza kuyatumia kwa shughuli za kilimo kuondoka mara moja hii ni kufwatia mgogoro ulionza kutokea baina ya wakulima na wafugaji katika eneo hilo huku akimtaka mkurugenzi wa halmshauri hiyo kuchukuwa hatua zaidi ikiwemo kuwapatia maeneo mengine . 

Mgumba ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo ambapo awali akizingumza na wananchi wanaoishi katika kijiji cha Msomera kusikiliza kero mbalimbali moja wapo ilikuwa ni pamoja na wavamizi waliotumia eneo lililotengwa na serikali kwaajili ya malisho na kuyatumia kufanya shughuli za  kilimo. 

"Eneo hili lilikuwa na poli tengefu, ni eneo la serikali yeyote aliyekuwa anaishi hapo alikuwa anaishi kinyume cha sheria na alikuwa ni mvamizi kama walivyo wavamizi wengine maeneo yote tuliyoyatenga kwa mujibu wa sheria kama yalikuwa ni malisho yaendelee kuwa malisho na wale wote walioolima kwenye maeneo hayo waondoke mara moja. alisema Mgumba.

 "Mkurugenzi wale watu ambao wamelima kwenye maeneo ya malisho au barabara kwanza waondolewe na kama hawana maeneo wakapimiwe maeneo sehemu nyingine wapewe hekali tano tano ili waendeleze kilimo kwenye maeneo yaliyotengwa kwaajili ya kilimo, maeneo yote tuliyoyatenga kwaajili ya huduma za kijamii yaendelee kubaki wazi kwa matumizi yaliyopangwa, na wafugaji waelekezwe na kupangwa katika maeneo kwaajili ya mifugo "aliongeza 

Hata hivyo amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya Handeni vijijini kwa kushirikiana na viongozi wengine kusimamia matumizi bora ya ardhi kama ilivyoelekezwa kisheria. Katika kijiji cha Msomera ambapo wanahamia kwa hiari wananchi wanaotoka katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorogoro tayari Serikali imetenga hekali mbili na nusu kwaajili ya makazi sambamba na hekali tano kwaajili ya kilimo kwa wote ambapo zaidi ya wananchi laki moja wanatarajiwa kuendelea kuhamia katika kijiji hicho. 

Awali akizungumza mwenyekiti wa kijiji cha Msomera Martin Paraketi amebainisha uwepo wa mgogoro baina ya wananchi waliohamia katika kijiji hicho kutoka Ngorongoro na waliowakuta wakigombania hasa maeneo kwaajili ya kilimo akiiomba serikali kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuondokana na athari ambazo zuinaweza kujitokeza baadaye ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe au wakulima na wafugaji.

 "Miongoni mwa changamoto tuliyonayo kubwa ni muingiliano kati ya wenzwetu waliohamia kutoka Ngorongoro na wenyeji waliowakuta baada ya mradi kupima maeneo mengi ya wenyeji yamechukuliwa hasa ukienda maeneo ya mashamba , mashamba ya wenyeji yote yamechukuliwa na hiyo ni changamoto kubwa kwa wote tunaomba msaada hiyo changamoto iondolewe ili wananchi wa kijiji cha Msomera waishi kwa amani na kuendelea na kufanya kazi zao kama watanzania wengine" alisema Paraketi. 

Akieleza katika upande wa elimu mwenyekiti huyo amesema kuwa katika shule ya msingi ya Samia Suluhu Hassan ambayo ni mpya licha ya uwepo wa miundombinu bado kuna uhitaji wa vyumba vingine vya madarasa hii ikilinganishwa na ongezeko la wanafunzi waliopo kwa sasa .

 Hata hivyo katika kutatua changamoto ya nyumba za walimu kwenye kiijiji hicho tayari serikali ilishaahidi kupeleka kiasi cha shilingi million mita tatu ambazo bado zipo kwenye mchakato.

 "Shule zetu tunazo mfano katika shule ya Samia ipo lakini hakuna nyumba hata moja ya walimu na pia kuna upungufu wa walimu lakini pia bado panahitajika madarasa mawili ya dharura idadi ya wanafunzi waliopo ni 876 sekondari ipo lakini watoto waliopo ni 176 , kila shule ina upaungufu wa walimu na madarasa japo serikali imejitahidi kutatua changamoto hizi lakini kutokana na ongezeko la watu nao uhitaji ni mkubwa" alisema . 

Kwa upande wake diwani wa Eyasi Ngorongoro Augustino Rumay Ginada ameipongeza serikali mara baada ya kuondoka kwa hiari hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia Msomera bado huduma za kijamii zinaendelea kuimarishwa huku akiomba kufikishiwa karibu huduma ya maji ambapo wakazi wa kijiji hicho hutembea umbali mrefu. 

"Tunaipongeza sana serikali na tuseme tu ukweli hatujajisikia vibaya na kujiona kama watoto yatima mara baada ya kutoka Ngorongoro tunajua tuko Tanzania na tunakaa kama watanzania wenzetu , lakini changamoto bado zipo tu sasa hivi bado maji tunayopata ni ya chumvi na tunayapata umbali mrefu tunajua jitihada za serikali lakini tunaomba basi tuangaliwe, upande wa maji ndio changamoto kubwa sana ambayo tunaipata kama wenyeji" alisema Diwani Rumay. 

Katika ziara yake mkuu wa mkoa Omari Mgumba alipata nafasi ya kutembelea mradi wa kituo cha afya Msomera ujenzi wa mnada pamoja na bwawa linalolosimamiwa na wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mkoa wa Tanga ambao yote kukamilika kwake itatoa huduma kwa wananchi wa kijiji cha msomera pamoja na vingine vya jirani vikiwemo Mzeri na Mbagwi.
Share To:

Post A Comment: