DENIS CHAMBI, TAGA

Timu ya mpira wa miguu kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania 'TAWA' imetangaza vita kubwa kwa wapinzani watakao kutana nao kwenye mechi zinazofuata hii ni baada ya kuwashushia mvua ya magoli 6-0 chuo cha usimamizi wa Biashara 'CBE' walipokutana katika mchezo wao michuano ya Shimuta uliofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya ufundi 'Tanga Tec'. 

Ushindi huo mnono walioipata TAWA ni wa kwanza tangu waanze kampeni hiyo kabla ya hapo wakitoka sare mbili kulisaka kombe la mwaka huu wa 2022 kupitia mchezo wa mpira wa miguu linaligombaniwa na timu mbalimbali kutoka mashirika ,kampuni na taasisis binafsi zinazoshiriki Shimuta mkoani Tanga. 

Kocha anayekinoa kikosi hicho Abdallah Msauka alisema kuwa ushindi wa leo ni marekebisho ya madhaifu yaliyojitokeza kwenye mechi zao mbili walizocheza na mchezo wao dhidi ya chuo cha CBE na ilikuwa ni lazima washinde mchezo huo ili waweze kuzisogelea zili nafasi mbuli za juu kuingia kweye hatua ya 16 bora.

 Alisema kadiri wanavyozidi kusogea mbele kwenye mashindano hayo ndivyo ugumu na upinzani unavyozidi kuongezeka hali ambayo inabidi wazidi kukiimarisha kikosi chao ili waweze kusonga mbele zaidia ikiwezekana kutimiza adhima yao ya kutwaa ubingwa kwenye mchezo huo na kurejesha furaha kwa waajiri wake . 

"Tunamshukuru Mungu mara baada ya kupata sare mbili tulisahihisha makosa yaliyojitokeza na mbinu tuliyowapa wachezaji wetu kwenye mchezo wa leo waliweza kuitumia na kupata ushindi mnono, kikubwa huu ni mwendelezo tunatakiwa tupambane tunajua waajiri wetu walitutuma ushindi wao walishafanya kazi yao na sisi tutahakikisha tunaingia 16 bora na mwishio wa siku tunafikia lengo la kutwaa ubingwa , tunajua kwamba tunakutana na timu ngumu lakini sisi tutajipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo tutakaocheza" alisema Msauka.

 Akizungumzia siri ya ushindi walioupata nahodha wa kikosi hicho Carlos Ernest alisema kuwa waliweza kuutawala mchezo hali ambayo iliwafanya wapinzani kupaki kibasi ili kupunguza idadi ya magoli lakini hata hivyo mbinu yao haikuweza kuwasaidia kitu hii ni kutokana na kuruhusu mashambulizi mengi waliyokuwa wakipelekewa langoni kwao.

 "Mashindano ni mazuri na mechi ya leo ilikuwa ni nzuri kwetu ukiangalia wapinzani walikaa nyuma ya mpira muda mwingi na lengo lao kubwa lilikuwa ni kupunguza idadi ya magoli kwa sababu walijua wanacheza na timu kubwa ambayo inacheza mpira wa kasi tunawashukuru sana waajiri na seikali kwa ujumla kupitia mashindano haya amabayo yanatukutanisha na ndugu zetu tunazidi kufahamiana zaidi,"
 alisema Ernest. 

Akizungumza mmoja wa wachezaji wa timu ya CBE Fredy Nchimbi amesema kuwa muda ambao wamecheza mchezo huo pamoja na hali ya hewa imekuwa sababu ya wao kupoteza kwa idadi kubwa ya magoli licha ya kuwa bado wana matumaini ya kuendelea kufanya vizuri katika mechi zao zilizosalia. 

"Tunakubali tumepoteza maana ni sehemu ya mchezo lakini tumekutana na changamoto ya kuchelewa kuanza kwa mchezo ukiangalia na hali ya hewa ya Tanga wachezaji wanakuwa wanachoka sana istoshe sisi ni wafanyakazi miili yetu haiawezi kuhimili , lakini bado tuna matumaini sisi bado ni wanajeshi tunaamini mechi mbili zilizobaki tutashinda" alisema Nchimbi. 

Mashindano hayo Shimuta yanaendelea mkoani hapa yanajumuisha michezo ya mpira wa miguu, Pete, wavu , kikapu , kukimbia na magunia, vishale , bao Draft, kuvuta kamba na mingineyo.
Share To:

Post A Comment: