Serikali imeteua Shule 56 za Michezo Tanzania Moja ya Shule hiyo ni Chief Sarwatt ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara kwa lengo la kuibua vipaji vya wanafunzi shuleni


Benson Maneno ni Afisa Michezo wa halmashuri ya Mbulu amesema kupitia shule hizo amesema uwepo wa shule maalumu za michezo kutasaidia kuinua vipaji vya watoto nakuweza kufikia ndoto ya kujiajiri kupitia michezo


Aidha Maneno amesema kuwa halmashauri hiyo imelipokea kwa furaha kwani tayari wameshampokea mwalimu wa michezo ambaye amepatiwa mafunzo kupitia wizara ya michezo na sanaa kwa kushirikiana na BMT.


"Halmashauri ya Mbulu tumejipanga vizuri kuhakikisha vipaji vya wanafunzi vinakua hasa kupitia shule yetu ya sekondari ya Chief Sarwatt lengo ni kupata wanamichezo  watakaotoka Mbulu  kwa lengo la kutuwakilisha kimataifa,"amesema Maneno.


Kwa upande wake Mwalimu wa michezo,Vicent Yahaya amesema mafunzo hayo yamewasaidia wao kutambua vipaji vya wanafunzi wanaopenda michezo pamoja kwa kutumia mbinu mbalimbali walizopatiwa ili kuwaanda watoto mazingira ya kupenda michezo.


Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo,wameiomba serikali kuingiza michezo katika mitaala ya elimu kwa lengo la kujengewa uelewa wa michezo tangu wakiwa wadogo.

Share To:

Post A Comment: