Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya ununuzi wa ndege mpya ya kunyunyiza dawa ya kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao.


Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Anthony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kishapu Nyangindu Boniface Butondo aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kununua ndege ya kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao hasa mtama na uwele katika mkoa wa Shinyanga.


Naibu Waziri Mavunde amesema katika mwaka huu wa fedha 2022/23 Serikali imetenga Shililingi Bilioni 3 kwa ajili ya ununuzi wa ndege hiyo ya kunyunyiza dawa kudhibiti wadudu waharibifu na kwamba mchakato unaendelea ili kujiridhisha na makampuni yaliyojitokeza kutoka zabuni hii ya ununuzi wa ndege.

Share To:

Post A Comment: