NA DENIS CHAMBI, TANGA
TAASISI ya Tanga Youth Tallent
Association (TAYOTA) imefanikiwa kutoa elimu ya ukatili kwa watoto wapatao elfu sitini (60,000) wa shule 108 za
msingi na sekondari zilizopo katika halmashauri ya jiji la Tanga hii ikiwa ni
jitihada za kuendelea kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia ambao unaendelea kushamiri katika jamii
mbalimbali hapa nchini.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa
taasisis hiyo ya TAYOTA George Bwire wakati
akizungumza kwenye semina ya waandishi wa habari wa mkoa waa Tanga inayolenga
kuwajengea uwezo wa kuandika na kuripoti habari bazihusu maswala ya jinsia
katika jamii semina ambayo pia ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka mahakama, vyama vya siasa,
jeshi la Polisi, TAKUKURU,viongozi wa dini, jeshi la Magereza na maendeleo ya
jamii kujadili pia namna jnsi ya kupambana na vitendo vya ki ukatili.
Bwire amesema kuwa dhamira ya
semina hiyo ni katika kutekeleza mradi wao unaolenga kutokomeza visa vya
ukatili kwa watoto na vijana waliopo katika rika balehe ndani ya jiji la Tanga
mradi ambao unafadhiliwa na shirika la Bortner
Foundation ambapo wamevipa kipaumbele vyombo vya habari kama nyenzo sahihi ya
kupeleka ujumbe kwa jamii juu ya mikakati wanayoenelea nayo ya kumbana na
kutokomeza ukatili katika jamii katika
kutoa elimu na hamasa kwa nia hiyo.
“Moja wapo ya vitu ambayo
tulitegemea kuvifanya katika huu mradi ni kujengea uwezo vyombo vyetu vya
habari kushiriki kikubwa ni kutoa elimu kwa jamii na watoto na shule zetu za msingi na sekondari ili
waweze kupata ulekewa juu ya ukatili ni nini kwa sababu kuna wengine hawalewei
hat, tumeoata nafasi ya kutoa elimu kwa shule zote za serikali za msingi na
sekondari zilizopo ndani ya jiji la
Tanga na tumeweza kuafikia wanafunzi Zaidi
ya elfu sitini na shule 108” alisema Bwire
Alisema kufwatia mradi huo mara
baada ya kufanya ufwatiliaji katika jamii imeonekana wazazi wamekuwa
wakishiriki kwa kiasi kikubwa kuchochea ukatili kwa watoto baadhi yao
wakiwashinikiza wanafunzi wa kike wasifaulu mitihani yao ili waweze kuwaozesha
hali ambayo inaweza kupelekea skuzima ndoto ao kielimu.
“Kabla ya mradi tulianza kutaka
kujua hali ya ukatili katika jamii ndani ya jiji la Tanga ipoje na hali
tulitoipata ni kwamba hali yenyewe sio nzuri watoto wengi wanapitia kwenye ukatili na hasa watoto 16 ambao
walishafanya mtihani wa darasa la saba wanasema hawako tayari kwa sababu
wameshaposwa wazazi wao wamewaambia maksudi wasifanye vizuri katika mitihani
yao ili waweze kuolewa na wengi
wanaowafanyia ni ndugu wa karibu , wapo walimu pia wanatemnea na wanafunzi hizi
taarifa” aliongeza.
Alisema bado katika jamii kuna
visa vingi vya ukatili havijaripotiwa mahali husika hivyo kupitia wanahabari
itkuwa ni njia moja wapo ya kuweza kuviibua na kuvitafutia ufumbuzi ili sheia
ziweza kuchukuwa mkondo wake na kunusuru kundi kubwa watoto ambao ni kizazi
kijacho.
Akifungua semina hiyo
itakayofanyika kwa siku nne mstahiki meya wa jiji la Tanga Abdurhaman Shillow amewahimiza wazazi kujua
na kutmbua majukumu yao katika malezi ya watoto kila siku kujenga ukaribu baina
yao na wazazi ili iwe rhisi kutambua matatizo wanayokumbana nayo na kuyapatia
ufumbuzi mapema
Aidha amewataka waaandishi wa
habari kutumia taaluma zao katika kuuga mkono jitihada za serikali kupitia
wadau mbalimbali kuweza kupambana na
vitendo vya ukatili kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vinavyohusika ili sheria
ziweza kuchukuliwa kwa wale wote wanaootekeleza vitendo hivyo
“Mkikaa kwenye semina hii vaeni
viatu vya matatizo yanayoikumba jamii kuna vishawishi vingi vijatumika
kuwapelekea watoto wetu kuingia katika ukatili wa kijinsia kuna watu sasa hivi
wanajirahisisha sana na wanapenda vitu vya bure ikiwemo hali ngumu ya kiuchumi matokeo yake matukio ya ukatili yamezoeleka na
yamekuwa kama ni kitu cha kawaida kitu
kingine ni utandawazi ambao ukiutumia vibaya utakuangusha sasa tujitafakari na
kuwaelimisha watu”
“Ni lazima wazazi wawe na
wasiwasi na watoto wao wasiwaache tu kama kondoo wasio na mchungaji ni lazima
wawe makini wafwatilie mienendo na kujua
marafiki wa watoto wao kila siku lakini wachukue tahadhari kwa mienendo na
hulka za watoto wao, lakini pia wazazi tuache vitisho kwa watoto wetu mtoto naweza
akashindwa kukuambia vitu vingine lakini kwa sababu umemtisha anashishwa kuja
kukuambia sasa ni lazima kuwa karibu kwa kujenga urafiki na watoto wetu”
alisema Shillow.
Akizungumza mwenyekiti wa chama
cha waandishi wa habari mkoa wa Tanga Lulu George ametaja maendeleo ya teknolojia
kuwa chanzo mojawapo kinachochangia kwa kasi kukithiri kwa vitendo vya ukatili
wakijinsia katika jamii akiwataka waandaandshi wa habari kuzidi kusimama imara
katika tathnia yao pamoja na kuandika taarifa zenye weledi ili kuweza kusaidia
kupunguza na kuondoa kabisa ukatili wa kijinsia huku akiwaomba wadau na
serikali kwa ujumla kutokulisahau kundi hilo katika Nyanja zote za kimaendeleo
kwa aajili ya maslahi mapana ya Taifa.
“Hali mbaya zaidi inazidi sasa
hivi tunapoona teknolojia imebadilika japo kuwa inaleta maendeleo kwa jamii
lakini kwa kasi kubwa inazidisha mmomomyoko wa maadili na mwenye jukumu kubwa
la kukemea hili ni sisi waandishi wa habari kwa kutumia vyombo vyetu vya habari
kwahiyo tujione kuwa ni sehemu ya jamii ambayo tunapaswa na tunahuska kuleta
mabadiliko tusimame katika nafasi zetu, lakini naomba waandishi wa habari, tusiachwe nyumba kwaajili ya mabadiliko
yanayohusu ndani ya jiji la tanga kuwe
na ushirikishwaji ili wote kwa pamoja tuweze kushirkiiana na kuleta yale
mabadiliko chanya kwa maslahi mapana ya jiji letu la Tanga na mkoa wetu kwa
ujumla”
Post A Comment: