Raisa Said, Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba  amezitaka Taasisi za
kifedha nchi kuendelea  kuwakopesha Wakandarasi Wazawa ili waweze
kutekeleza miradi yao kwa wakati.

Wito huo ameutoa wakati wa semina kwa wateja wa Bank ya CRDB
iliyofanyika mjini Tanga na kuhudhuriwa na wateja  zaidi ya 1000.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa miongoni mwa wafanyabishara na
Wakandarasi wengi walikuwa wanakosa kazi na wengine kazi zao zilikuwa
zinasuasua kutokana na ukosefu wa mitaji. Alisema kwamba mashariti ya
Serikali kuwapa kazi ni lazima wawe na fedha ya kuanzia kutekeleza
mradi huo.

Mgumba alieleza kwamba wengi waliokuwa na mitaji midogo walikuwa
hawetekelezi kwa wakati  na miradi mingi ilikuwa inachelewa.

“Nawapongeza Bank ya CRDB kwa kuamua kuwapa mikopo wakandarasi wakubwa
hadi sh.billion 20  na pia wakandarasi wanaweza kuungana watano au
kumi  wakapewa mitaji ya kutosha kitu ambacho kimeondoa changamoto
hiyo ya mitaji, " amesema Mgumba

Mkuu huyo wa Mkoa amesema pia bank hiyo mwanzo ilikuwa inawapa
wajasiriamali wadogo  kama vile mama lishe, baba lishe na
wafanyabishara wa sokoni mikopo ya  sh.50 million.  Sasa hivi,
amesema, wameongeza hadi sh 2 billion.

Pia amesema kuwa katika bajeti hii inayoendelea r Serikali imetenga
bajeti ya sh trillion  3.8  kwa ajili ya Wizara  ya Ujenzi  na kati ya
hiyo Sh tillion 1.4 ni kwa ajili ya sekta ya ujenzi  hivyo fedha ya
kuwalipa wakandarasi watakaopata kazi kwenye miradi kwenye barabara na
 kwenye viwanja vya ndege na mingine yote fedha za kuwalipa  zizo.
Aliitaka bank ya CRDB iendelee kuwakopesha.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki hiyo Abbdulmajid Nsekela alileza kuwa
Benki hiyo imeandaa semina hiyo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali
ili kuwaleleza fursa zilizopo ikiwepo pamija na uoanuzi wa Bandari ya
Tanga na bomba la Mafuta.

Amesema upanuzi wa bandari utasababisha kuogeza kwa mizigo
inayopakuliwa na kusarifisha kupitia bandari ya Tanga jambo ambalo ni
fursa kwa  wafanyabiashara na wajasiriamali.

Mkurugenzi huyo pia amesema kuwa benki imeanzisha bidhaa nyingine

inayoitwa mbegu ambayo inawalenga wajasirimali wanawake na vijana mabo wana mawazo ya ubunifu  ambapo watapatiwa mitaji(mikopo) kwa ajili yakuendeleza mawazo na biashara zao.
Share To:

Post A Comment: