Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania,  ipo mbioni kutengeneza sera ya huduma za maktaba ikiwemo marekebisho ya sheria ya mwaka1975 ili kuendana na kasi ya utoaji huduma hizo  kwanjia ya kieletroniki kitaifa na kimataifa.

Akizungumza katika mafunzo ya siku tano yanayofanyika Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) yaliyokutanisha wataalam wa maabara za kisayansi kupitia Shirikisho la Maktaba na Vyuo vya Utafiti (COTUL) ,Mkurugenzi wa Bodi hiyo,Dkt. Mboni Ruzegea alisema sera hizo zikirekebishwa pamoja na sheria itatoa wigo mpana wa kazi zinazofanywa na watunzi wa vitabu ikiwemo wahadhiri na watafiti kutambulika zaidi kupitia maktaba za kieletroniki.

Pia wanafuzi kuanzia ngazi za chini hadi vyuo vikuu wataweza kusoma mambo mbalimbali kupitia  maktaba hizo katika viganja vyao vya simu au kompyuta mtandao sehemu yoyote watakapokua kwaajili ya kujisomea vitabu au vitu mbalimbali vilivyotungwa na watanzania na watunzi wengine kimataifa

"Huduma za maktaba ni bure lakini tukiungana kwa pamoja na vyuo vikuu mbalimbali wasomi watasoma vitabu kupitia mfumo wa kieletroniki ambao ni rafiki kwa kila mtu na sheria hii ikirekebishwa pamoja na sera tutafika mbali kupitia maktaba za kieletroniki"

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (IAA)Dkt ,Cairo Mwaitete alisema endapo vyuo vikuu vikiungana kwa pamoja na mfumo huo wa kieletroniki ukianza kazi watu mbalimbali watasoma vitabu ikiwemo tafiti za wahadhiri na maprofesa zinazoweza kusomwa na kupata ufumbuzi wa jambo husika.

Alisema endapo COTUL na Wizara ya Elimu zikiungana kwa pamoja gharama za uchapishaji vitabu zitapungua ikiwemo kila vyuo kuwa na maktaba za kisasa ili kuongeza wanachuo, wanafunzi na watu mbalimbali kusoma vitabu kwaajili ya manufaa yao.

Awali akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango alisisitiza watanzania kupenda kusoma vitabu ili kujifunza mbinu mbalimbali za kimaisha ikiwemo wanafunzi na wanachuo katika vyuo mbalimbali.

Alisisitiza maabara hiyo ya kieletroniki itasaidia watunzi wavitabu kujulikana ndani na nje ya nchi kwani watajulikana kimataifa na kitaifa kutokana na utunzi wa vitabu vitakavyosomwa kwanjia ya eletroniki.









Share To:

Post A Comment: