Na Zanura Mollel, LONGIDO

Chama Cha Mapinduzi wilayani Longido Mkoa wa Arusha Kimemtangaza Ndugu Papa Nakuta Mollel kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho baada ya kumuangusha aliyekua Mwenyekiti wa Chama hicho miaka mitano iliyopita Ndugu Joseph Ole Sadira kwa asilimia 50.13.

Uchaguzi huo ulifanyika hapo Jana ambapo wagombea walikuwa ni Joel Maumba aliyepata kura 12,Joseph Ole Sadira 384 na Papa Nakuta 398 kura zilizoharibika zikiwa 09,hivyo kura halali zilizopigwa zilikua kura 782.

Akimtangaza Mwenyekiti huyo , msimamizi wa Uchaguzi kutoka ngazi ya Mkoa Yasmin Bachu ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake  Chama Cha Mapinduzi Mkao wa Arusha(UWT) alisema uchaguzi huo ni wa wazi na wagombea wote wamesaini fomu ya kukubali matokeo.

Akizungumza Papa Nakuta baada ya Ushindi aliahidi kusimamia ahadi zake ya kuhakikisha ongezeko la matawi ya Chama hicho kwenye kata zenye  upungufu pamoja na kuhakikisha anawaunganisha wanachama na kuvunja siasa za kikoo,Ukanda,Rika na Ukabila.

" Wanalongidodo wote ni sawa hakuna mrefu wala mfupi sote ni sawa na ahidi kusimamia usawa na haki ndani ya Chama hiki" alisema Nakuta.

Joseph Ole Sadira ambaye alishindwa kutetea kiti chake kwa Pungufu ya kura 14 alimshauri Papa Nakuta kufanya kazi Kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali waliopo wilayani hapo Kama Chama kinavyoelekeza pamoja na kuhakikisha anavunja makundi yaliyojitokeza kipindi hiki Cha uchaguzi.

" Mdogo wangu Papa nikupongeze kwa ushindi huu,miaka ya nyuma na Mimi nilikua nikiwaburuza wengine Leo na Mimi nimeburuzwa nimekubali ila Nakuomba ukakisimamie Chama kusiwepo na mipasuko wajengee umoja Wana CCM" alisema Sadira.

Joel Maumba aliahidi kufanya kazi na Mwenyekiti Mpya kwa lengo la Kujenga na kukiimarisha Chama hicho,huku akiwataka wanaCCM kumuunga Mkono Papa Nakuta kwa kumpatia ushirikiano kutokana na Wajumbe kuonyesha lmani kubwa kwake.

Wakati huo huo uchaguzi wa Katibu wa itikadi ,Siasa na uenezi ilifanyika ambapo Mwandishi wa habari Solomon Lekui aliibuka mshindi kwa kura 59 na katika sera yake aliahidi kukiunganisha Chama na Vyombo vya habari katika utendaji kazi.

" Kura zilizopigwa zilikua ni 98 ,wagombea walikua watatu Jacob Lepasi alipata kura 28 na Yohana Laizer 08"alidai Papa Nakuta.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: