Tumbaku hukuzwa kwaajili ya majani yake,majani ya tumbaku yanapo komaa huvunwa na tumbaku hutumika hasa kutengeneza sigara.
aina za tumbaku zinazo limwa Tanzania ni fire-cured tobacco na flue cured-tubacco,fire cured tobacco hulimwa kusini mwa Tanzania hasa Ruvuma na flue cured tubacco hulimwa Tabora, Iringa na Rukwa.

HALI YA HEWA NA UDONGO

   Tumbaku huitaji kiasi cha 38mm cha mvua ambayo imenyesha vizuri katika kipindi cha wiki 16 baada ya kupanda au kuhamishia miche shambani (transplanting) mvua nyingi hua na madhara huchochea kupatkana kwa magonjwa.
   Flue cured- tobacco husitawi vizuri katika udongo mwepesi (loamy) na udongo wa kchanga (sandy), na haiitaji udongo unaop tuamisha maji na pia huitaji nitrogen katika hatua za mwanzo na kadri inavo zidi kukua huitaji wa nitrogen hupungua.udongo unapokua na nitrogen nyingi wakati wa majani kukomaa ubora wa majani hupungua.
  Tumbaku husitawi vema katika maeneo yenye mwinuko toka usawa wa bahari 900m hadi 1500m, japo kua fire cured-tobacco haistawi vizuri kwenye maeneo yenye mwinuko 1400m kutoka usawa wa bahari.

KUANDAA SHAMBA

Tengeneza matuta yenye umbali wa 1m, pia zingatia kuzika magugu yote na tengeneza matuta mapema katika kipindi cha mvua ukifanya hivyo itasaidia kuamishia miche shambani mapema katika kipindi cha mvua.

KUTENGENEZA VITALU

  Zingatia kutafuta eneo zuri na salama la kuweka vitalu na lazima liwe karibu na chanzo cha maji, kama eneo lipo sehemu ambayo kunaupepo mkali zingatia kutengeneza kikata upepo.badilisha upande wa kuweka vitalu kila mwaka kuzuia wadudu waalibifu (nematodes).

  tengeneza vitalu vilivo inuka viwe na upana wa 1.2m na urefu wa 23m. Baada ya kutengeneza matuta tifua udongo uwe katika size ndogo na baada ya hapo nyunyuzia dawa ya kuuwa nematode kwa kufata maelezo kwa usahihi yalio andikwa katika chupa ya dawa.


  kabla ya kupanda weka mbolea ya NPK katika vitalu ukichanganya na udongo kwa kutumia rake,
na baada ya kuweka mbolea chukua kane na weka maji safi ndani yake kisha weka mbegu ndani ya kane hiyo na kisha nyunyuzia maji na mbegu katika kitalu kwa usahihi na baada ya hapo changanya kwa kutumia rake tena.


  baada ya hapo wekea nyasi vitalu vyako na kisha mwagilia kila siku mara tatu na utatoa nyasi hizo pale unapoona mbegu zimeanza kuota kwaanzia wiki ya 3 na kuendelea. baada ya mbegu kutokeza na kuondoa nyasi unamwagilizia mara moja kwa siku na wiki 2 kabla yakhamishia miche shambani mwagilia mara 1 kwa siku mbili ili kuwezesha miche kuhimili ukame, na miche hua tayari kwa kuamishiwa shambani baada ya wiki 8 toka kupandwa.


hamishia miche shambani inapofikisha urefu wa 15 cm na zingatia usafi wa mikono na mavazi wakati unafanya kazi katika vitalu vya tumbaku na pia hepuka kuvuta sigara ukiwa shambani.

KUPANDA

Tumbaku hupandwa kwa kutumia mbegu, mbegu hupandwa katika vitalu na huamishiwa shambani pale inapo fikisha urefu wa 15cm
  mwagilia miche wakati wa asubuhi au jion na ng'oa miche kwa umakini ili kuepusha kukata mzizi mkuu(tap root).
 tengeneza mashimo katika matuta na kama unapanda fire cured tubacco mashimo hutakiwa kua na umbali wa 1m na kama unapanda flue cure tubacco umbali wa mimea hua 54cm hadi 59cm na kama mashimo ni makavu mwaga lita 1 hadi 2 za maji kwakila shimo, zingatia kuacha mzizi mkuu ukiwa wima.

PALIZI

Palilia shamba pale magugu yanapo anza kutokeza shambani na rudia mara kwa mara, wakati wa kupalilia zingatia kurudisha udongo kwenye mmea.

MBOLEA

weka mbolea ya NPK wiki moja baada ya kupanda na unatakiwa kuweka kinacha 10cm na umbali wa 10cm  toka kwenye mmea.

KUKATIA(topping)

Pale unapoona mmea mmoja kati ya mitano imeanza kutoa maua unatakiwa kukata maua hii itasaidia sana kuongeza ukubwa wa majani ambayo ndio tumbaku inayoitajika.

DE SUCKERING

Pale mimea inapokua imeondolewa maua hutengeneza kitu kinacho itwa sucker, ondoa hiyo saka kabla haijafika urefu wa 15 cm.
Share To:

Post A Comment: