Na Imma Msumba;Monduli


Zaidi ya wanafunzi 190  wa kidato cha kwanza katika  shule ya sekondari engutoto wilayani monduli mkoani arusha wamekosa malazi baada ya bweni lao kuteketea kwa moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana  na hivyo kulazimika kulala katika madarasa . 

Mbunge wa Monduli Fred Lowasa ametoa pole kwa mkuu wa shule ya sekondari Engutoto, walimu wa shule hiyo, wazazi, wanafunzi pamoja na wanamonduli kwa ujumla kwa janga la moto lililotokea siku ya jumamosi 17/82022.

Jumamosi tulikuwa kwenye mazishi kule kata ya Lashaine na wakati tunatoka tukapigiwa simu kwamba kuna moto katika shule ya sekondari Engutoto. Tuliwahi tukamkuta mwalimu mkuu pamoja na viongozi wengine wa wilaya waliokuwa wamefika kushirikiana kuzima moto, wakati huo zimamoto walipigiwa simu na kufika kwa wakati na kutusaidia katika kuzima kwani moto ulikuwa mkubwa sana. Alisema

Aidha aliwashukuru na kuwapongeza sana jeshi zima moto kwa kuweza kufika kwa wakati kutoka Arusha mjini na kuwasaidia kuzima na kuokoa baadhi ya vitu. Pia ametumia nafasi hii kuisisitiza serikali  kuwa sasa wilaya ya Monduli nayo inahitaji gari ya zima moto kwasababu majanga kama haya yakitokea kama ni usiku ingekuwa hatari.

Afisa elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Magreth Muro pia amewashukuru wadau wote waliojitokeza kuwasaidia katika janga hilo. Afisa elimu huyo alisema kuwa wapo watu waliojitokeza kuwasaidia akiwemo mbunge wa Monduli Mheshimiwa Fred Lowasa ambaye ameshirikiana na shirika la msalaba mwekundu katika kutoa magodoro mia mbili (200) mablanketi mia mbili (200) pamoja na neti mia mbili (200).

Vilevile wapo wengine waliojitolea kuwasaidia akiwemo mkurugenzi aliyejitolea kuweka vioo  na mwingine kujitolea kuweka sakafu katika bweni ambalo halijakamilika lengo likiwa ni kuwasaidia watoto kuweza kupata bweni la kulala. Zaidi ya hayo amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kutatua  changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Kwa upande wa wanafunzi walionusurika na janga hilo la moto wamesema kwa sasa wanatumia madarasa nyakati za usiku kwa ajili ya malazi huku asubuhi yakitumika kwa masomo. Aidha wameshukuru sana kwa msaada huo waliopatiwa.


Share To:

Post A Comment: