MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema  anatambua uwepo wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) pekee.

Kutokana na hali hiyo amewaonya baadhi ya maofisa wa Jiji la Arusha wanaopita shule mbalimbali kutangaza kuhusu chama kingine cha walimu.

Mongella ameyasema hayo wakati akizindua miongozo mitatu ya uboreshaji wa  elimu Mkoa wa Arusha

Amesema baadhi ya watumishi wa Jiji la Arusha, idara ya elimu wanapita kuhamasisha walimu kujiunga na chama ambacho serikali haikitambui.

Amesisitiza hataki migogoro mkoani kwake  na kusisitiza walimu kupendana, ikiwemo maofisa elimu kuacha kupanga safu za waratibu elimu kata au wakuu wa shule, wasiojua maana ya kuchafuka na chaki, kukosa viti au changamoto mbalimbali za walimu.


H.T ; Habarileo

Share To:

Post A Comment: