Waumini wa makanisa mbalimbali wilayani Hanang mkoani Manyara wametakiwa kutangaza na kueneza taarifa juu ya utumiaji sahihi wa barabara ikiwemo kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza vifo vinavyoendelea kutokea kutokana na uzembe usio wa lazima

Hayo yamesemwa na kamanda wa kikosi cha usalama  Barabarani Wilaya ya Hanang Inspekta Volca Willa wakati akizungumza na waumini wa kanisa la Sabato hukj akisema kuwa utii wa sheria za alama barabarani itasababisha kupungua kwa ajali japo barabara zina changamoto chache na serikali inashughulikia sehemu zilizo na changamoto katika barabara hizo

Kwa upande wake mchungaji wa kanisa hilo Nkunu Jeshi amesema kuwa wao tayari wameanza kutoa elimu hiyo na kwa sasa wameanzia kutoa elimu kwa watoto hivyo wataandaa utaratibu mzuri wa kuanza kutoa elimu kwa waumini wote.
Share To:

Post A Comment: