Watu 20 wamefariki dunia  na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka Kahama mkoani Shinyanga.


Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea majira ya jana jumatatu saa nne usiku Agosti 8,2022 ikihusisha gari ndogo IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta. Inaelezwa kuwa Hiace imegongana uso kwa uso na Lori/Scania yenye namba za usajili T658 DUW.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Kahama watu 20 wamepoteza maisha na 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.


"Watu 17 walipoteza maisha papo hapo eneo la tukio na watatu wamefariki baada ya kufikishwa hospital,majeruhi wapo 15", taarifa inaeleza.


Mpaka sasa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga halijazungumzia kuhusu tukio hili,juhudi za kumtafuta Kamanda wa polisi zinaendelea

Share To:

Post A Comment: