Diwani Winjuka Songelaeli Mkumbo akiwa katika pozi enzi za uhai wake.

Vijana wa Green Gurd wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba mkoani Singida wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Diwani wa Viti Maalum wa Tarafa ya Kinampanda, Winjuka Songelaeli Mkumbo wakati wakiupeleka kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika Kijiji cha Simbalugwala Kata ya Mukulu jana. Diwani Winjuka alifariki dunia kwa ajali ya gari Agosti 17, 2022 baada ya Basi la Tanzanite lenye namba za usajili T 916 DNU alilokuwa akisafiria kutoka Singida kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka Mlima Saranda uliopo Wilaya ya Manyoni na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa.

Marehemu Winjuka Songalaeli Mkumbo enzi za uhai wake.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakiwa wamejipanga tayari kwa kuelekea ibada ya mazishi ya mwenzao Winjuka Songalieli Mkumbo yaliyofanyika jana Kijiji cha Simbalugwala.

Madiwa hao wakiwa tayari kwa ajili ya ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Singida Kaskazini, Noel Lameck.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora akiongoza msafara wa madiwa kwenda kwenye ibada hiyo. 
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa tayari mbele ya eneo maalum ilipofanyika ibada hiyo.
Mme wa marehemu, Winjuka,  John Lyanga akiwa na huzuni kubwa wakati wa ibada hiyo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Mkoa wa Singida, Prisca Maleta anayeishi Manyoni ambaye alishuhudia ajali hiyo akizungumzia tukio hilo
Vijana wa Green Gurd wa CCM wakiwa tayari kwa lolote wakati wa ibada hiyo.
Huzuni wakati wa ibada hiyo.
Mjomba wa marehemu ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Ndugu ya Sweden Mzee Amoni Gyunda akifarijiana na baadhi ya ndugu wakati wa ibada hiyo.
Ni huzuni tupu.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ni huzuni tupu ya kuondokewa na mpendwa wao. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Singida, Diana Chilolo na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iramba, Samuel Ashery wakati wa ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Ni huzuni tupu katika ibada hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mwalimu Ephrahim Kolimba akiwaekeleza masuala ya itifaki vijana wa Green Gurd wakati wa ibada hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mwalimu Ephrahim Kolimba (kulia) akiwa na Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya hiyo, Abbas Michael wakati wa ibada hiyo.
Chakula kikiwa tayari wakati wa ibada hiyo.
Taswira ya ibada hiyo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Iramba ambao walikuwa wakiwezeshwa na marehemu Winjuka kupitia Taasisi ya Ndugu ya Sweden wakiwa kwenye ibada hiyo. Watoto zaidi ya 900 walikuwa wakisaidiwa na taasisi hiyo.
Katibu wa Kanisa la T.A.G Singida Kaskazini,  Mchungaji Danford Mlumba, akisali wakati akiuombea mwili wa marehemu kabla ya kufanyika ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni wakati mwili wa marehemu ukipelekwa kwenye ibada hiyo.
Mwangalizi wa kanisa hilo , Joel Masinsi akiongoza itifaki za ibada hiyo.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) wilayani humo,  Glory Chubwa akiongoza wimbo maalum katika ibada hiyo.
Ibada ikendelea.
Samson Shila akisoma wasifu wa marehemu.
Katibu wa Kanisa la T.A.G Singida Kaskazini,  Mchungaji Danford Mlumba, akizungumza katika  ibada hiyo.

Askofu Noel Lameck akiongoza ibada hiyo.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko, akitoa salama za rambirambi za mkoa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomola akizungumza katika ibada hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk.Mwigulu Nchemba akitoa salamu za rambirambi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akitoa salamu za rambirambi.
Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mjomba wa marehemu Mzee Amon Gyunda ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Ndugu ya Sweden akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mwanfamilia ya marehemu, Evaline Lyanga, akitoa neno la shukurani.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Singida, Diana Chilolo, akimpa pole Mbunge wa Iramba Magharibi, Dk.Mwigulu Nchemba.
Pole zaidi zikitolewa kwa Dk.Mwigulu.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos  wakati wa ibada hiyo ya mazishi ya Winjuka Mkumbo.
Umati wa watu ukisubiri kwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Foleni ya kwenda kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Vijana kutoka Wilaya ya Iramba wakiwa kwenye ibada hiyo. Kulia ni  Mdau Ahmed Makame. 
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foeni kwenda kuuaga mwili wa mpendwa wao Winjuka Mkumbo.
Ni huzuni tupu katika ibada hiyo.
Taswira ya uegeshaji wa magari wakati wa ibada hiyo.


 

Na Dotto Mwaibale, Singida


AJALI ya Basi la Tanzanite lenye namba za usajili T 916 DNU  iliyoua watu tano mkoani Singida imeibua mapya baada ya mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo kueleza kuwa mabasi yanayofanya safari kati ya Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam madereva wamekuwa wakishindana kufika mapema kwa kuchochewa na  bonasi inayotolewa na matajiri wa magari hayo.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Mkoa wa Singida, Prisca Maleta anayeishi Manyoni mkoani hapa ambaye alikuwa mtu wa kwanza kushuhudia ajali hiyo na kutoa msaada kwa majeruhu na kuzistiri maiti.

Maleta aliyasema hayo jana kwenye ibada ya mazishi ya Diwani Viti Maalum wa Tarafa ya Kinampanda Wilaya ya Iramba Winjuka Mkumbo ambaye alikuwa ni miongoni ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

"Mimi ni Mwanaharakati nilifuatilia jambo ili na nilipoongea na Winjuka eneo la ajali aliniaambia mwendo wa basi hilo tangu linaondoka Singida ulikuwa mbaya kwani dereva alikuwa akiendesha kwa kasi na kusababisha abiria kuanza kutafutana na walipofika Manyoni abiria walimkataa na akaanza kuendesha dereva mwingine wa akiba ambaye naye alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi kuliko yule wa mwanzo hadi tairi lilipopasuka na kusababisha ajali" alisema Maleta.

Alisema alipofuatilia kwa karibu aligundua sababu ya mwendo kasi wa mabasi hayo ni madereva hasa wa mabasi ya kutoka Mwanza kugombea mnara yaani anayekuwa wa kwanza kufika anapewa bonasi na matajiri wa mabasi hayo.

"Tunaomba Serikali kuliangalia jambo ili kwani matajiri wengi wanawapatia madereva wao minara na wa kwanza kufika ndiye atakayepewa bonasi na suala  la pili ni wale watu wanaofika eneo la ajali tukiwaamini kwa asilimia 100 ndio wanakuwa wa kwanza kuwafilisi kwa kuwaibia majeruhi na watu waliopoteza maisha kwani nimewashuhudia kwa macho yangu na wanangu wakiwafunua zile nguo zetu tulizowa wasitiri kwa kuwafunika na kuanza kuingiza katika mifuko yao na kuchukua fedha na vitu vingine vya thamani kwa kuwa tunawafahamu baadhi yao majina tumempa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni  kwa ajili ya kushughulikia suala hilo" alisema Maleta.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga vituo vya afya, zahanati na Hospitali lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi pale wanapokuwa wagonjwa na kupata ajali lakini amesikitishwa na kitendo cha majeruhi wa ajali hiyo kuona wakipoteza maisha licha ya kuwepo huduma za hospitali karibu na eneo la ajali.

"Ajali imetokea mlima Saranda, pale Kintinku pana zahanati,Maweni pana Kituo cha afya na Manyoni pana Hospitali ya wilaya ni umbali wa kilomita zisizozidi 20 kwa nini hawa majeruhi wasingepelekwa katika maeneo hayo kwa ajili ya kupata huduma ya kwanza ambayo ingesaidia kuzuia damu zisitoke badala yake wakawachukua na kuwapeleka Dodoma umbali wa zaidi ya kilometa 150 bila usaidizi wowote na baadhi yao kujikuta wakipoteza maisha akiwepo diwani Winjuka" alisema Killimbah.

Killimbah alitumia nafasi hiyo kutoa agizo kwa Serikali kuhakikisha inaaliangalia jambo hilo kwa karibu na kuwa itakuwa haina maana kuwa na zahanati, vituo vya afya, hospitali kila mahali lakini wananchi wanapoteza maisha kwa kuwasafirisha umbali mrefu kwa ajili ya kuwapatia matibabu huku wakikosa huduma kwenye maeneo ya karibu ambazo zingesaidia kuokoa maisha yao.

Katika mazishi hayo simanzi na vilio na watu kuzimia vilitawala huku kila mtu akimzungumzia marehemu Winjuka Mkumbo kwa jinsi alivyokuwa akijitoa kusaidia jamii katika Wilaya ya Iramba na maeneo mengine ya jirani.

Akiongoza ibada ya mazishi Askofu Noel Lameck wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Singida Kaskazini alisema umati wa watu uliokuwepo katika ibada hiyo unaonesha jinsi  Winjuka Mkumbo alivyokuwa akiishi vizuri na jamii na kanisa na akatumia ibada hiyo kumuomba kila mtu kujiandaa kwa kutubu na kuokoka.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Iramba Michael Matomora akitoa salamu  za rambimbia aliagiza kila siku kuhakikisha gari lake linakuwa limewekwa mafuta  ili kusaidia kusafiri wakati wote hasa kunapokuwepo na jambo la dharura.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi alisema halmashauri hiyo tangu itokee ajali hiyo na kumpoteza diwani wao Winjuka Mkumbo imetoa ushirikiano na kugharamia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakihitajika.

Miongoni waliopata fursa ya kumzungumzia marehemu Winjuka ni pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko ambaye alitoa rambirambi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Uchumi , Dk.Mwigulu Nchemba, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau, Wajumbe wa Kamati ya Siasa kutoka wilaya ya Iramba na Mkoa wa Singida wakiwepo, Diana Chilolo, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Ahmed Kaburu.

Makundi mengine yaliyopata fursa ya kutoa rambirambi zao na kumzungumzia marehemu Winjuka ni vikundi vya wananawake vilivyokuwa vikisaidiwa na marehemu, wanafunzi zaidi ya 900 waliokuwa wakisomeshwa na kusaidiwa na marehemu kupitia Shirika la Ndugu la Sweden, watu binafsi, makanisa mbalimbali na taasisi zingine zilizopo wilayani humo.

Marehemu Winjuka Songalieli Mkumbo alizaliwa tarehe Oktoba 6, 1974 katika Kijiji cha Simbalugwala ambapo alihitimu darasa la saba mwaka 1989 na kufunga ndoa na John Lyanga katika Kanisa la T.A.G Mwaka 1991.

Enzi za uhai wake marehemu ameshika nyazifa mbalimbali katika kanisa na maeneo mengine na hadi anafariki alikuwa Diwani wa Viti Maalum wa Tarafa ya Kinampanda wilayani Iramba mkoani Singida.

Marehemu Winjuka Mkumbo alifariki Agosti 17, 2022 kwa ajili ya gari iliyotekea Mlima Saranda wilayani Manyoni na ameacha mme, watoto watatu, wawili wa kike na wakiume mmoja Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amen. 

 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: