Jamii imeaswa kupanda miti yenye kutunza uoto wa asili na kuhifadhi mazingira kwa ujumla ilikuendana na mabadiliko ya tabia nchi yanayo endelea kuikumba dunia kwa ufanyaji wa shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na yaliyo hifadhiwa ambapo shughuli hizo za kibinadamu zinazofanywa husababisha athari za kimazingira kama ukosefu wa mvua na ukame katika maeneo mengi ya nchi.
Mkuu wa wilaya ya Mafia Mkoani pwani Injinia Martine Ntemo ameyasema hayo alipo tembelea banda la wakala wa huduma za misitu Tanzania katika maonyesho ya wakulima , wavuvi na wafugaji nanenane kanda ya mashariki yenye mikoa minne ya Tanga, Pwani , Dar es salaam na mwenyeji Morogoro.
Dc Martine Ntemo amewataka wakala wa huduma za misitu tanzania (TFS) kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa upandaji wa miti ilikuepukana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ya nayoendelea kuikumba dunia kwa sasa.
Pia amewaomba wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuendelea kuhamasisha upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya nchi na uhifadhi wa mazingira kwa kutunza vyanzo vya maji ilikuepukana na mabadiliko ya tabia nchi yaliyo sababishwa na shughuli za kibina damu.
Kwa upande wa Meneja msaidizi kanda ya Mashariki msimamizi wa rasilimali za misitu amesema wao kama wakala wa huduma za misitu tanzania wanaendelea kupanda miti katika mashamba yao na kuzalisha miti ambayo hutolewa kwa wananchi ilikupanda katika maeneo yao hivyo amewaom ba wananchi luendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yao.
Post A Comment: