Na Mwandishi Wetu.

Kampuni namba moja kwa utoaji wa huduma za Kidigitali nchini , Tigo Tanzania Leo Agosti 5 , 2022 imezindua duka jipya na la kisasa Eneo la Kisasa - Merriwa Jijini Dodoma duka litakalotoa huduma zote za Kidigitali kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani Ndani ya Jiji hilo.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Duka hilo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa huduma nzuri na Bunifu mbalimbali walizonazo zenye lengo la kutoa huduma za kidigitali na kurahisisha maisha ya watanzania walio wengi, ikiwa ni sehemu ya adhima ya serikali ya kuhakikisha Watanzania  wanafikiwa na kunufaika na ulimwengu wa Kidigitali 


Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri ( aliyesimama ) akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Duka Jipya la Tigo Jijini Dodoma

" Tigo mmefanya jambo kubwa kwa wakazi wa Kisasa na Jiji la Dodoma kwa Ujumla maana sasa wananchi hawatahitaji kwenda mjini kufuata huduma na bidhaa za Tigo ambazo hapo awali zilikuwa zikipatikana katika maduka ya Tigo yaliyoko mjini tu , Duka hili litawasaidia wananchi wa eneo hili kuepuka usumbufu wa kusafiri kufuata huduma kwa maana nimeambiwa duka hili litatoa huduma kama uuzaji wa simu janja  , Intaneti ya Nyumbani pamoja na ubadilishaji wa SIM, Tigo Pesa, huduma za usajili upya wa kibayometriki n.k hakika haya ni mapinduzi makubwa hongereni sana Tigo " . Alimalizia 

Naye kwa upande wake Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Bwn. Daniel Mainoya  amesema “uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa Tigo wa kuboresha utoaji wa huduma huku ikitimiza ahadi yake ya kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa bora na huduma kwa urahisi zaidi JiJINI Dodoma ”.


Duka hili jipya litaweza kuhudumia hadi watu 300 kwa siku lakini pia  lina eneo maalum la matumizi ambapo wateja wanaweza kupata fursa ya kufanya majaribio na kupata uzoefu wa bidhaa mbalimbali za Tigo kama vile simu za mkononi kabla ya kuzinunua.


Ahadi yetu kwa wateja ni kuwapa huduma za kibinafsi katika duka moja kwa mahitaji yao yote. Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma zetu kunatokana na hitaji la wateja kufuata mtindo wa maisha wa kidijitali kote nchini. Mpango wetu ni kutoa masuluhisho jumuishi kama sehemu ya mkakati wetu wa kuendesha ushirikishwaji wa kidijitali katika ukanda huu” alimalizia Bwn. Mainoya







Share To:

Adery Masta

Post A Comment: