Na,Jusline Marco;Arusha


Serikali imesema kuwa imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuongeza miundombinu ya kupima na kutibu magonjwa ya saratani kwa kuweka za CCT SCAN katika kila hospitali za mikoa.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu,katika Kongamano la 1 la Kimataifa la Saratani lililofanyika jijini Arusha Mkurugenzi Mtensaji wa Taasisi ya Saratani Ocean road Dkt.Julius  Mwaiselage amesema kuwa uginjwa wa saratani umekuwa ukiongezeka kwa kasi nchini kutokanana ulaji wa vyakula vya kisasa.

Aidha Dkt.Julius amesema kuwa  katika kuhakikisha jitihada hizo zinafanikiwa serikali imewezesha huduma za kuchunguza ugonjwa wa saratani zinapatikana katika hospitali zote za kanda na za mikoa ikiwemo tiba ya saratani ya upasuaji na tiba kemia ambapo tiba ya mionzi inaendelea kuboreshwa nchini.

Ameongeza kwa kukitaka chama cha madaktari bingwa kuhamasisha madaktari waliomaliza vyuo na ambao wanafanya kazi kujiunga katika program za ikolojia ili kuweza kutatua changamoto ambayo imeonekana ya wataalamu na madaktati bingwa upande wa ikolojia nchini kwani tayari serikali inatoa ufadhi wa kozi hizo.

"Takwimu inaonyesha kwamba wapo madaktari bingwa wa ikolojia wapatao 38 nchini ambao hawatoshi ukilinganisha na idadi ya kubwa ya wagonjwa kwani daktari mmoja anahudumia karibu wagonjwa 1200 ambapo tunatamani takwimu ziwe chini ya wangonjwa 100."alisema Dkt.Julius


Vilevile amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kusambaza huduma ya upimaji kupitia mashine za CCT SCAN kupitia mradi wa IMF ambapo hospitali zote za mikoa zitakuwa na mashine hizo.

"Hii inamaanisha kwamba badala ya mgonjwa wa saratani aende kwenye hospitali za Kanda kifanyiwa uchunguzi ataenda kwenye hospitali za Mkoa kipata huduma hiyo na hii inamaanisha kuwa huduma za CCT SCAN zinasogezwa karibu na wagonjwa.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa  takwimu  walizonazo asilimia 33 ya wagonjwa wanaopatikana nchini hufika kwenye vituo vya afya kwa ajili ya tiba kwani changamoto ya magonjwa yasiyoyakuambukiza ndiyo yanayoongoza nchini.

"Ukiangalia miaka kumi au kumi na tano iliyopita magonjwa ya kuambukiza ndiyo yaliyokuwa mengi ikiwemo malaria na kifua kikuu lakini kutokana na maboresho mbalimbali ambayo serikali imeyafanya kwa wananchi imepelekea kubadilisha maisha ya wananchi katika ulaji wa vyakula."aliongeza Dkt.Julius

Kwa upande wake Daktari bingwa wa saratani na rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Saratani Tanzania Dkt.Jerry Ndumbaro amesema ugonjwa wa saratani umekuwa ukiongezeka kwa wingi na kufanya idadi ya wagonjwa kuwa kubwa ambapo katika takwimu za mwaka jana wagonjwa zaidi ya elfu 42 wanapatikana kwa mwaka ambapo lengo la kongamano hilo ni kubadilishana utaalam kwa wataalam wa ndani na nje ya Tanzania ili kuboresha huduma katika eneo la saratani.


Amesema kama chama kinahakikisha wanawawezesha wataalam na watoa huduma za afya ngazi za mikoa na wilaya kupata utaalam wa kuweza kugundua magonjwa hayo mapema na kutoa matibabu kwa wagonjwa ambapo mpango walionao ni kufanya huduma za upimaji na ugunduzi wa mapema wa saratani katika jamii.

Ameongeza kwa kueleza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa mitindo ya maisha ikiwemo kutokufanya mazoezi,uzito uliopitiliza,ulaji mbaya wa vyakula,ni miongoni mwa dalili hatarishi za uwepo wa magonjwa wa saratani ambapo ameitaka jamii kuhakikisha inabadili mitindo ya maisha yao ili kuweza kujikinga na saratani.


Hata hivyo Kongamano hilo limejumuisha wataalam na washika dau katika eneo la saratani wakiwemo madaktari bingwa,wauguzi,watoa huduma za mionzi pamoja na makampuni ya dawa.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: