Na John Walter-Manyara

Leo Julai 20,2022 ni kilele Cha maadhimisho ya siku ya Idadi ya watu Duniani.

Maadhimisho hayo yanafanyika Uwanja wa shule ya Msingi Katesh B wilayani Hanang’ mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi ni waziri wa fedha Mwigulu Nchemba aliyemwakilisha waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Katika salamu zake kwa wananchi amesisitiza juu ya umuhimu wa watu kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi Agosti 23 mwaka huu kwa kuwa ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi na taifa.

Wananchi,viongozi wa dini,Siasa, taasisi na mashirika mbalimbali yamehudhuria.

Kamishna wa Sensa Tanzania Bara Anne Makinda amesema kuwa, Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ya kisasa na bora zaidi kwa kuwa imepangwa kufanyika mpaka ngazi ya kitongoji tofauti na ile ya 2010 iliyofanyika kwa kuishia ngazi ya wilaya.

Amesema kuwa,wameweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kila mtu anahesabiwa kwa wakati na kwamba kila kituo kitatumia kuhesabu kaya 50.

 Makadirio ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu ulimwenguni yanaonesha kwamba hadi kufikia mwezi Novemba idadi ya watu inatarajiwa kufikia bilioni 8 duniani,huku India ikitajwa kuipuki China ifikapo 2023. 

Hadi sasa nchi zote mbili India na China zina idadi sawa ya watu bilioni 1.4, lakini kulingana na ongezeko la vizazi nchini India huenda likaipiku China kufikia mwaka 2023.

Idadi ya watu duniani  inakadiriwa kuwa bilioni 8 kufikia novemba Novemba 15 mwaka huu na inaweza kufika bilioni 8.5 ifikapo mwaka 2030, bilioni 10.4 kwa mwaka 2100, kutokana na kupungua kwa kasi ya idadi ya vifo, ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliotolewa siku ya Jumatatu imesema.

Kauli mbiu inasema” Dunia ya watu Bilioni nane kuhimili wakati ujao ni fursa ya haki kwa wote,shiriki Sensa kwa maendeleo endelevu”.

Share To:

Post A Comment: