Wakii wa kujitegemea na Makamu Mwenyekiti wa MISA – TAN James Malenga akitoa mada kwa waaandishi wa habari za Mtandaoni kuhusu Sheria za Mtandaoni na sheria ya Huduma za habari katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyofanyika leo Julai 20,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bw. Deodatus Balile akifafanua jambo katika semina ya Sheria ya Huduma za Habari 2019 iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ili kuwapa uelewa kuhusu sheria hiyo ambayo imefanyika kwenye hoteli ya Sapphire jijini Dar es salaam Leo Julai 20, 2022. 

 Baadhi ya waandishi wa habari za mtandao wakiwa katika semina ya Sheria ya huduma za habari 2019 iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kufanyika kwenye hoteli ya Sapphire Leo Julai 20, 2022 jijini Dar es Salaam.Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari za mtandao wakiwa katika semina ya Sheria ya huduma za habari 2019 iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kufanyika kwenye hoteli ya Sapphire Leo Julai 20, 2022 jijini Dar es Salaam.

 

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Anitha Mendoza akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Wakili James Malenga kwenye Semina hiyo.


 


MAKAMU Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA–TAN) Wakili msomi wa kujitegemea James Marenga amesema
Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni ya mwaka 2019, inaweza kumtia mtu hatiani na hatimaye kumfunga hata kama hakufika mahakamani ili kusikilizwa.

Ameongeza mtu anaweza kushtakiwa na kupelekwa mahakamani bila yeye kuwepo na akahukumiwa na kufungwa halafu ndio akatafutwa na kukamatwa kisha kupelekwa gerezani bila kujua kesi yake ilipelekwa mahakamani lini, na kwa kosa gani.

Kutokana na maelezo hayo amesema ndio maana Iko haja kwa wadau mbalimbali wa sekta ya habari wanaona iko Sheria ya Uhalifu wa Mtandao ya mwaka 2019 inatakiwa kupitiwa upya.

Wakili Marenga ameyasema hayo leo Julai 20,2022 katika semina ya siku moja ya waandishi wa Habari za mtandaoni iliyofanyika katika Hoteli ya Sapphire Jijini Dar es Salaam,ambapo amefafanua Sheria hiyo Kifungu cha 50(2)(b) kinaondoa haki ya mtu kukata rufaa kinyume na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba.

Lakini pia Kifungu cha 38(2)(b) cha sheria hii kinaruhusu usikilizwaji wa shauri mahakamani hata bila muhusika kuwepo."Hii inaweza kumnyima mtu haki ya kusikilizwa na kujieleza kwa sababu kesi itaendeshwa mahakamani hapo akiwa hayupo maana yake hataweza kujitetea au kujieleza jambo ambalo linazuia haki ya mtu kujieleza na kusikilizwa".

Ametumia nafasi hiyo Wakili Marenga kueleza kuwa kwenye sheria hiyo kuna adhabu zilizowekwa kwa makosa ambayo hayapo wazi kinyume na Ibara ya 13 (6)(C) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni wajibu wa wadau mbalimbali kutoa maoni yao kuhusu sheria hiyo ili ifanyiwe marekebisho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile amewataka waandishi wa habari za mtandao kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao kuhusu sheria ya Huduma za habari ya mwaka 2019 ili kuhakikisha inarekebishwa.

Katika semina hiyo washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari za mtandaoni wameshiriki ambapo wamepata nafasi ya kuelezwa masuala mbalimbali yanayohusu Sheria hiyo, ambayo imeelezwa Kuna kila sababu ya wadau kutoa maoni yao kwa lengo la kuhakikisha inaboreshwa kwa kuondoa vipengele ambavyo vinaonekana ni kandamizi.
Share To:

Post A Comment: