WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maji wa Jamhuri ya Watu wa India Gajendra Singh Shekhawat lengo likiwa ni kuleta salam za shukrani kwa Serikali ya India kutokana na sapoti pamoja na mikopo nafuu inayotolewa kwa Serikali ya Tanzania kutekeleza miradi ya maji nchini 

Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Maji wa Shinyanga-Igunga-Shelui unaotoa Maji katika ziwa Victoria ambao umejengwa na kukamilika kwa muda uliopangwa na sasa Miradi ya miji 28 inayoendelea kutekelezwa maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Jumaa katika mazungumzo hayo ameeleza pamoja na kushukuru hizo ameomba kuimarishwa zaidi mashirikiano baina ya Wizara ya Maji India na Wizara ya Maji Tanzania. 

Ameanisha maeneo ya kipaumbele ya mashirikiano hayo kuwa ni ufadhili wa miradi mingine ya maji; Kuwajengea uwezo zaidi Wataalam wetu wa Sekta ya Maji katika nyanja za Usanifu na Ujenzi wa Mabwawa, rasilimali za maji na kuandaa maandiko ya Miradi Mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso ametumia fursa hiyo kuelezea nia thabiti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kupeleka huduma ya Maji yenye kutosheleza katika Majiji ya Dodoma kwa kutoa Maji katika Ziwa Victoria na Dar Es Salaam kutoa Maji mto Rufuji. 

Hivyo, amewasilisha ombi kwa Serikali ya India ya kufadhili miradi hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Maji India Gajendra Singh Shekhawat ameeleza kuwa serikali ya India ipo tayari kuendelea kushirikiana na kuisapoti serikali ya Tanzania kwenye miradi mbalimbali na kuonesha faraja kubwa kwa Mhe Aweso kufika Wizarani kwake na kuahidi yote waliozungumza kufanyiwa kazi na kuhakikisha yanatekelezwa.Share To:

Post A Comment: