Dodoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Godfrey Chongolo ametoa wito kwa ngazi zote za Watendaji kuanzia Tawi,kata, Wilaya na Mikoa yote Nchini kuwekeza nguvu kwenye uwekezaji na utendaji wa uchumi wa chama.


Ameyasema hayo Julai 13,2022 katika Kongamano la Mafunzo  ya Uongozi na uwajibikaji katika mada za Itikadi,Elimu ya Sensa na makazi,Tehama na Usajili wa Wanachama pamoja na Masuala ya Ulinzi na Usalama kwa Viongozi wa Chama kuanzia ngazi za Mashina Jijini Dodoma.


Amesema uboreshwaji wa uchumi kwenye chama itasaidia mambo yote kuwa rahisi na wataepuka kukimbiana katika vikao vya kujenga masuala yote ya msingi.


" Ni lazima kwanza tuboresha uchumi ili mambo yatunyookee, tukiboresha uchumi wa chama chetu mambo yetu yote yatakuwa rahisi na tutaacha kukimbiana kwenye masuala ya Msingi",amesema 


"Na hivi karibuni tutakusanya mikoa ambayo imelala lala tunawachukua waje kujifunza waone Mikoa mingine inavyofanya vizuri Mkoa wa Dodoma ni moja kati ya Mikoa inayofanya vizuri katika suala la Uchumi".Amesema Chongolo


Aidha amesisitiza kwa Wagombea kuepuka suala zima la rushwa  katika kipindi hichi cha uchaguzi ikiwi ni kiapo cha Mwanachama ambapo ni ahadi katika chama.


"Tunaposoma ahadi ya Mwananchama kila Mmoja aliapa kuwa rushwa ni adui wa haki na pale mlikuwa mkimaanisha kuwa rushwa ni jambo lisilokubalika,kila Mmoja atumie yale mema yake ambayo anaona ataweza kujinadi ",smesema


"Tufanye Kampeni kwa kutumia nguvu  zetu bila kutengenezeana  uongo na uzushi pamoja na kutengenezeana ajali tusipende kuwekeana chuki sisi kwa sisi".Amesema Chongolo


Hata hivyo  Chongolo ameagiza vikao vitakavyo jadili majina ya wahusika katika ngazi usika kutoona aibu kuchukua hatua kwa watu watakao kiuka maagizo halali yaliyowekwa na Chama.


"Hatuwezi kuwa chama ambacho tunatoa maelekezo kwaajili ya kutoa fursa kwa Watu wote kuwa sawa kwenye kugombania kinyang'anyiro cha kugombea nafasi mbali mbali na baadhi ya wachache kuona wao wanapembe ndefu kuliko Mmiliki wa pembe usika",amesema


"Chama ndicho  chenye dhamana na nafasi, Mtu ukiona unataka  dhamana hiyo usipo fuata maagizo na maelekezo yetu utakuwa hututakii jambo zuri na utakuwa unatulazimisha kuchukua hatua na hatutosita kuchukua kwasababu utakuwa ameyataka mwenyewe".Amesema Chongolo

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: