Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) leo imetoa maamuzi kuhusiana na sekretarieti kufungua kesi katika kamati hiyo dhidi ya afisa habari wa Yanga Haji Manara.

Kamati ya maadili ya TFF imemkuta na hatia Haji Manara na kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi na faini ya Tsh milioni 20 kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia

Haji Manara alipishana kauli na Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

Share To:

Post A Comment: