NA REBECA DUWE, TANGA

WAZIRI Wa Afya Ummy Mwalim amewataka watanzania kuweka nguvu kubwa katika kufanya usafi wa Mazingira ili kuweza kuweka nguvu katika kinga badala ya tiba kwani kinga ni bora hivyo ni wajibu wa kila mwanajamii kufanya usafi wa mita tano katika eneo lake.


Hayo aliyasema wakati akizindua mpango wa taifa wa  Afua ya Unyinyiziaji wa viuadudu vya kibaiolojia kwenye mazalia ya Mbu katika ukumbi wa halmasahauri ya jiji la Tanga ambayo ilifanyika kitaifa mkoani  humo.


Waziri Ummy alisema kuwa pamoja na Afua ya viuadudu watanzania wote wanapaswa kuweka nguvu katika usafi wa mazingira kuhakikisha mazalia ya mbu yanatokomea ili kudhibiti malaria.


“Kila mwanajamii one umuhimu wa kutumia Afua hii  ili kuweza kuangamiza mazalia ya mbu ili lengo la serikali la kutokomeza malaria ifikapo 2030 iweze kutimia “. alisema Waziri Ummy


Awali akiuzungumzia mpango  na utekelezaji huo kaimu meneja wa mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria Tanzania Dr . Samweli  Lazaro  alisema mradi huo ni wa miaka miwili ambapo  kwa katika  mkoa ulioweza kupata bahati na kutimiza vigezo ni mkoa wa  Tanga.


Alisema wameanza kutekeleza kwa kuzingatia udhibithi wa malaria  ambapo mikakati ya kuangamiza mazalia ya mbu  kwa lengo kuu ikiwa ziro malaria hapa nchini.


“Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria  kwa kushirikiana shirika la uswiss TPH kupitia Mradi wa TEMT unaofadhiliwa na serikali ya Uswiss umepanga kutekeleza  Afua ya Kuangamiza viluilui vya mbu katika mazalia ya  ili kudhibiti  malaria na magonjwa mengine yaenezwayo na mbu, kama Dengue,Homa ya manjano , Homa bonde la Ufa , Matende na Mabusha.” Alisema Lazaro.


 Naye mkuu wa mkoa wa Tanga Adam Malima alisema kuwa katika mkoa wa Tanga Halmashauri iliyopata vigezo hivyo ni tatu ambapo ni halmashauri ya wilaya Tanga mjini , wilya ya Handeni na Wilaya Lushoto. 


Alisema kwa miaka hiyo miwili mradi huo utatekelezwa ndani wilaya hizo s, sambamba  na hayo alimuomba waziri Ummy kuwa kutokana mbu kusafiri vyema wilaya za jirani halmashauri ziweze kufikiwa na Afua hiyo.


Kwa upande wake balozi wa Uswis nchini Tanzania Didier Chassot alisema kuwa serikali ya uswiss iliamua kufadhili mradi huo kwa kuona umuhimu mkubwa wa kudhibiti malaria kwa watanzania.


Hata hivyo alisema serikali ya Uswiss ipo tayari kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha Tanzania inakuwa na ziro malaria.


Naye Dr.Adiel Mushi ambaye ni mwakilishi wa Taasisi ya umoja wa marais wa Afrika dhidi ya malaria (Alma ) alisema kuwa wako tayari kushirikia na na serikali katika mapambano dhidi ya malria na kuhakisha wanatoa nguvu katika kuhamasisha  kutunza mazingira kwa kuondoa mazalia ya mbu.

Share To:

Post A Comment: