Na,Jusline Marco:Arusha


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Suleiman Msumi amekabidhi jumla ya kilo 500 za mchele katika vituo 10 vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi vilivyopo kwenye halmashauri ya Arusha ikiwa ni awamu ya pili ndani ya mwezi mmoja kwa Mhe.Rais kutoa masaada wa vyakula kwa watoto yatima katika halmashauri hiyo.

Akikabidhi vyakula hivyo,Msumi amesema kuwa serikali inathamini sana mchango mkubwa unafanywa na asasi za kiraia kwa kutekeleza malengo ya serikali katika sekta ya Ustawi wa jamii husani kwenye malezi ya watoto yatima jambo ambali limemfanya Mhe.Rais kuyoa chakula hicho ili kuwahudjmia watoto hao kutokana na malezi hayo kuwa ni jukumu la serikali, kwa kuthamini kazi hizo.

"Mhe.Rais ametoa kilo 500 za mchele kwa vituo 10 vyenye jumla ya watoto 255 wanaoishi kwenye vituo hivyo, niseme tu kwamba Mhe. Rais anawajali na kuwathamini watoto yatima, anatamani watoto hao watimize ndoto zao kama ilivyo kwa watoto wengine wenye wazazi". Amesistiza Mkurugenzi Msumi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakikabidhiwa chakula hicho,walezi wa vituo hivyo wamekiri kuwepo kwa uhaba wa vyakula kwenye makazi ya kulelea watoto yatima kwa sasa ambapo zoezi hilo limefanyika kwenye ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo.


"Tuseme tu wazi kuwa kwa kutupa chakula hiki Mhe.Rais amewanusuru watoto yatima kwa njaa kutokana na ukweli kwamba kwa sasa vituo vyetu vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyakula na mahitaji mengine ya kila siku." Wamesistiza viongozi  wa vituo hivyo.

Aidha licha ya kumshukuru Mhe.Rais kwa msaada huo wa chakula kupitia serikali ya awamu ya sita, walezi wa vituo hivyo wamesistiza kuwa chakula hicho kimekuja wakati muafaka kutokana na kuwepo kwa tatizo la upungufu wa vyakula katika makazi mengi ya kulea watoto yatima kwa sasa.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Huruma Ophanage kilichopo kijiji cha Kiserian kata ya Mlangarini, Yohana Msomba amebainisha kuwa kwa sasa vituo vya watoto yatima vinakabiliwa na uhaba wa vyakula na mahitaji mengine ya kila siku hali inayotokana na vituo vingi kutegemea wafadhi kutoka nje ya nchi ,wafadhili ambao wamesitisha kuleta misaada kutokana na athari za UVIKO 19, Vita vya Ukraini pamoja na ukame.


Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha Shalom Center, Glory Swai ameipongeza serikali kwa kutoa elimu bila malipo jambo ambalo limepunguza gharama kwa vituo vya watoto yatima sambamba na kuwawapa fursa watoto yatima kusoma vizuri kama watoto wengine na kutimiza ndoto zao.

"Nikiri wazi kuwa msaada huu ni wa thamani na ynaweka alama kubwa sana kwa watoto inaonesha jinsi ambavyo serikali inawajali watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, tunaishukuru serikali kwa kuwapenda na kuwajali watoto wenye uhitaji" Amesisitiza Dkt.Alex Lengeju Mkurugenzi wa Kituo cha Kanani Ophanage Kilichopo Kisongo.

Hata hivyo Afisa Utawi wa Jamii Kiongozi halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi amesema kuwa kutokana na ufuatiliaji unaofanywa na ofisi yake umebaini makazi ya eatoto yatima kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa chakula na mahitaji mengine kwa kuwa baadhi ya wafadhili waliokuwa wakitegemewa kutoa misaada kusitisha huduma hiyo jambo lililosababishwa na athari za UVIKO 19 pamoja na vita vya Ukraini.

Vilevile ameitaka jamii kushirikiana na serikali kujitoa kuwalea watoto wanaoishi kwenye makao kwa kutoa msaada wa kitu chochote walicho nacho ili kuvinusuru vituo hivyo sambamba na kuisisitiza jamii kuona umuhimu wa kuwalea watoto yatima katika familia zao.



Share To:

JUSLINE

Post A Comment: