Mbunge wa jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amefanya ziara ya Kusikiliza kero za Wananchi kupitia Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Lendikinya Kata ya Sepeko .


Awali Akisoma Risala mbele ya Mbunge ,Kereto Moipan Amesema kijiji cha Lendikinya kuna miradi Mingi yanayoendelea ni pamoja na Ujenzi wa  Madarasa Shule ya msingi Lendikinya na imekamilika kwa asilimia 99.


“Changamoto zipo nyingi ikiwemo Ukosefu wa maji  na Hii ni kwa sababu ya Malimbikizo ya bili ya maji kuwa kubwa kwa sababu ya mita Kusoma Monduli na si Kijiji husika, Miundombinu ya bomba mbunge tunaomba marekebisho ya na bomba, mh mbunge Mikopo kwa kina Mama ni changamoto kubwa hawa kinamama nao wana haki sawa na wengine tuangalie kwa hili”. Amesema Kereto.


Kwa Upande wa Mwanachi mwingine Miseyeki Kipuyo amesema Mashamba ya lendikinya yaliyopo broaris ni Mali ya kijiji cha Lendikinya lakini Mapato yanaenda Halmashauri badala kwenye account ya kijiji, “swala la umeme ni changamoto pia kwa sababu imefika kwenye kijiji  lakini haijasambazwa kwenye vitongoji vyote vitatu vya lendikinya Mh Mbunge hili nitakuuliza mwaka 2025 juu ya utekelezaji wake Swala la Maji Mh mbunge kati ya Changamoto utakazoipa Suluhu Angalia swala la Maji Lendikinya hili nalo tutakuuliza 2025”.miseyeki 

Akijibu Changamoto hizo Awali mbunge Fredrick Lowassa Ameahidi ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Sepeko Ambapo kijiji cha Lendikinya ni miongoni mwa vijiji vinavyounda Kata hiyo.

“Swala la migogoro ya Ardhi ni Aibu sana kama sisi wenyewe tunagombana kwa Ardhi yetu ambayo sisi wote ni ndugu nikuombe Mzee Mong’i mwenyekiti kijiji cha Lendikinya simamia hili kwa haki na usawa , “ishu ya Maji Imeelezwa  vizuri juu ya AWUSA NA RUWASA , Mimi mradi ambao niliomba Serikalini Kipindi cha Hayati Magufuli  ni Mradi wa vijiji 13 unatoka kwenye tank kubwa la  Ngorbob inapita Barabarani ,Moita ,Meserani unakuja hadi Nanja , huu mradi ni wa Billioni 4.8 umefanyiwa study nimerizika ikatokea changamoto ya mashindano kati ya RUWASA NA AWUSA, jana tulikaa kikao na Wanasema RUWASA ndo wamefanikiwa kupata huo mradi na huo mradi utatangazwa Wiki ijayo , kwa hiyo nikifanikiwa na mradi huo Lendikinya mtapata Maji ya kutosha , kwa hiyo mradi huo unakuja na maji lendikinya tutazungumza kwa ujumla wake baadaye.”mbunge Fredrick Lowassa.


Share To:

Post A Comment: