Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Taifa (SHIUMA), Ernest Matondo akitoa taarifa kwa Umma kupitia Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu kutowatambua baadhi ya watu wanaojitambulisha kuwa ni vongozi wa Machinga. Kushoto ni Msemaji wa SHIUMA Taifa Zeche Zabron na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Vijana SHIUMA, Catherine John.

....................................................

Na Alex Sonna-DODOMA

UONGOZI wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) umesema kuanzia leo hautambui wala hawatahusika na chochote kwa wale wanaojitambulisha kama ni viongozi wa SHIUMA bila uhalali wa nyadhifa wanazozitaja.

Kwa mujibu wa tamko walilolitoa leo Juni 2,2022 jijini Dodoma kupitia kwa Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa Ernest Matondo Masanja amesema kuwa hautambui wala hatuhusiki na kikundi cha watu wanaojitambulisha kama viongozi wa SHIUMA.

“Bila uhalali wa nyadhifa wanazozitaja ikiwemo Machinga Saccos LTD, Gazeti la la Wamachinga na kudai kumiliki taasisi inayotambulishwa kama “Machinga Media Group”.

Amewataja wanaojitambulisha ni Lusinde Steven kama Mwenyekiti,Yusuph Namoto Mwenyekiti wa SHIUMA Dar es salaam,Augustino Choja Naibu Katibu Dar es salaam.

Wengine ni Mohammed Nchigamo Mwekahazina wa Dar es salaam,Masoud Chauka Katibu wa Mkoa wa Dar es salaam,Shaban Matwebe Mshauri wa Machinga dar es salaam

“Watu hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakijishirikisha na vitendo vya utovu wa nidhamu ndani ya chama vilivyosababisha Mkutano Mkuu wa SHIUMA kuwavua madaraka kupitia maazimio ya wajumbe waliokutana Jijini Dodoma tarehe 19 Mei, 2022.

Amesema Mkutano huo pia uliweka viongozi wa mpito katika nafasi hizo hadi uchaguzi Mkuu utakapofanyika ambao ni Christopher Kidiga Mwenyekiti Dares Salaam.John Mbagwile Makamu Mwenyekiti Dares Salaam,Marcelina Mijingo Katibu SHIUMA Dar Es Salaam

Wengine ni Kelvin Josephat,Naibu Katibu Mkuu Dar Es Salaam,Mohamed Aali,Mweka Hazina Dar Es Salaam,Ismail Faisal Afisa Habari/Msemaji wa MachingaDar Es Salaam.

“Kwa tamko hili SHIUMA inapenda kuutahadharisha Umma wa Watanzania wakiwemo wanachama wa shirikisho hili, wadau na Taasisi mbalimbali za kifedha wasishirikiane wala kujihusisha na shughuli za kikundi cha watu hao kwa kuwa hawatambuliki na shirikisho.

“Kwa tamko hili natarajia Umma wa Watanzania utatoa ushirikiano kwa SHIUMA ili kukidhi matakwa na maono ya viongozi wetu Wakuu walio na kutuwekea mazingira mazuri kwa mstakabali wa Taifa,”amesema.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: