Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Kaika Saning'o Ole Telele akijiandikisha tayari kuondoka kwa hiari ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuhakimia katika kijiji cha Msomera,Handeni mkoani Tanga.



 NIMEAMUA kwa hiyari yangu! Ndivyo anavyoeleza aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha Kaika Saning'o Ole Telele baada ya kuondoka kwa hiari ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro.

Akizungumzia kuhusu hatua aliyochukua kuondoka kwenye eneo hilo ,Ole Telele amesema huo ni uamuzi wake na familia yake na sasa wanahamia wilayani Handeni kwenye Kijiji cha Msomera ambako wakazi waliokuwa wakiishi Ngorongoro wamehamia huko kwa hiyari 

Amesema kwamba ni vema wakazi wengine wa Ngorongoro kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya Taifa na vizazi vijavyo kwa kulinda na kuhifadhi mazingira ya eneo la hifadhi.

Hatua ya Ole Telele imekuja ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa zoezi la kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro wanahama kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi hiyo na kuhamia katika eneo la Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Pamoja na mambo mengine ametoa mwito kwa wakazi wengine walioko Hifadhi ya Ngorongoro  kuhama kwa hiari ili kuruhusu shughuli na uhifadhi kuendelea katika eneo hilo.

Kwa upande wake Mkuu kuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amemsifu Ole Telele na kueleza kwamba uamuzi wa viongozi kama yeye utasaidia kuhamasisha wananchi zaidi kuondoka katika eneo hilo ambalo ni urithi wa dunia.

Aidha amesema hadi sasa  jumla ya kaya 48 zenye wakazi 228 zimeishahama katika eneo la Ngorongoro na kuhamia katika kijiji cha Msomera ili kupisha uhifadhi wa ikolojia wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro."Wakazi walioko katika eneo hili la hifadhi wameendelea kujiorodhesha ili kuondoka kwa hiyari , tunawapongeza kwa kufanya uamuzi sasa.



Mbunge wa zamani wa Jimbo Ngorongoro Mhe. Kaika Saning'o Ole Telele akielezea  utayari wake wa kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga.



Share To:

Post A Comment: