Na John Walter-Manyara

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto nchini DCP Marry Nzuki ameitaka Jamii  kuacha kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili waweze kutimiza ndoto zao za baadaye.

Amezungumza hayo Kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika  ambayo kwa mwaka huu kitaifa yalifanyika kata ya Orkesumet wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambapo amezitaka jamii ambazo bado zinashikilia mila potofu kuacha mara moja kwani ndio kisababishi Cha vitendo hivyo.

Aidha Nzuki amewataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuwapa haki zao za msingi.

Naye kamanda wa polisi mkoa wa Manyara ACP Benjamim Kuzaga amesema katika jitihada za kuendelea kukomesha vitendo hivyo, jeshi la Polisi kitengo Cha dawati la jinsia na watoto mkoani humo wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuacha mila potofu zinazochangia watoto kufanyiwa Ukatili kupitia mashuleni,minadani na Kwenye Mikutano ya hadhara.

Kauli mbiu ya siku ya Mtoto wa Afrika mwaka 2022; Tuimarishe ulinzi wa mtoto,tokomeza Ukatili dhidi yake,jiandae kuhesabiwa. 

Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Mwaka tarehe 16 Juni baada ya kupitishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) ambapo Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa Umoja wa Afrika imekuwa ikiadhimisha siku hii tangu mwaka 1991.

 Lengo la kuadhimisha siku hii ni kukumbuka mauaji ya kinyama waliyofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mwaka 1976. 

Share To:

Post A Comment: