Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameiasa Halmashauri ya Mafia,kubuni vyanzo na kuweka mikakati mipya ili kuinua uchumi na kujiongezea mapato ya ndani.


Alitoa Rai hiyo wakati wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani cha Kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ,kilichofanyika Ukumbi wa Magereza Wilayani Mafia.

Licha ya hayo, Kunenge ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kupata Hati safi kwa Miaka 6 Mfululizo huku akiwaasa wasibweteke kwa kuridhika na hati wanazozipata.

Ameeleza Zamani Halmashauri zilikuwa zinapata Ruzuku Kubwa lakini kwa sasa Serikali imewapa Miradi Mikubwa ya Kimkakati , pamoja na kutakiwa kuibua vyanzo vipya Ili waweze kujiendesha.

"Nione zaidi Mikakati Mipya ya Kuongeza Mapato kama Mikakati ni ile ile Bajeti ni ile ile hatuwezi kuwa na matokeo mapya kwa kuwa Bajeti ni mipango unayoipa gharama ,alisisitiza Kunenge.

Ameelekeza Madiwani hao wapatiwe Mafunzo ya Uchumi ili waweze kuwa Wabunifu wa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kutumia Ipasavyo Fursa za Uchumi na Uwekezaji katika Halmshauri hiyo.

Kunenge aliwataka kwenda na Spidi ya Rais Samia Suluhu Hassan,"Spidi ya Rais ni kubwa sana anatafuta Wawekezaji je akileta Wawekezaji Mafia ,"tunachakuwapa alihoji Kunenge.

Kuhusu Migogoro ya Ardhi kwenye Halmashauri hiyo Kunenge alisema kuwa ameombea fedha Serikalini ili kisiwa Chote kipimwe na kupanga mji.

"Tunataka kisiwa hiki kiwe eneo zuri sana baadhi ya vitu tulivyonavyo tunaongoza Duniani, Mafia ni Lulu Amesema Kunenge.

Amemwelekeza Katibu Tawala Mkoa kufuatilia Hoja zote zilizojirudia na kuwachukulia hatua wote waliosababisha Hoja hizo, na Halmashauri ifunge Hoja zote zilizo ndani ya Uwezo wao ifakapo Septemba 30 na kupitia Sheria ndogo na kufanya marekebisho.

Nae Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Juma Salum Ally amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuitangaza Mafia, amesema kuwa wamefanikiwa kudhibiti Ukusanyaji wa Mapato ambapo wameongeza kutoka Shilingi Milioni 900 walizokuwa wanakusanya mwaka jana hadi Bilioni 1.3 mwaka huu.

Mkaguzi Mkuu wa Nje Mary Dibogo Ameeleza kuwa Halmashauri hiyo kwa mwaka wa Fedha 2020/21 ,Hoja zilizotakiwa kujibiwa ni 54 na hadi sasa zimejibiwa 24 na kubaki 30.
Share To:

Post A Comment: