ARUSHA.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha,Seleman Msumi ameishukuru Serikali kutoa magari kwa halmashauri zote nchini,ikiwemo halmashauri yake,kwa ajili ya kufuatilia miradi inayotekelezwa na TASAF katika halmashauri hiyo.

Msumi ametoa shukurani hizo kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu kwa kutoa gari hilo kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri ambapo amethibitisha kuwa gari hilo litarahisisha ufuatiliaji wa miradi katika vijiji 88 vya halmasahuri hiyo vinavyotekeleza mradi wa Kunusuru kaya Masikini.


Aidha amesema kwa jiografia ya halmashauri ya Arusha, kuna maeneo ambayo hayafikiki kwa haraka hivyo uwepo wa gari hilo utawarahisishia watalam kuifikia miradi na walengwa kwa urahisi na kwa wakati.

Vilevile amesema jambo hilo litairahisisha serikali kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kaya zenye uhitaji zinazohudumiwa na TASAF.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: