Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Nd. Jerry C. Muro leo tarehe 28/06/2022 amewaweka Kikaaongoni Viongozi wa Kamati ya Ujenzi wa Vyoo vya Shule ya Msingi Issuna Baada ya Wajumbe wa Kamati hiyo Kugoma Kuidhinisha Fedha za Ujenzi Huo kwa Madai ya Kutoshirikishwa Kwenye Maamuzi.


Akizungumza Wakati Ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika kata ya isuna kijiji cha isuna B katika Shule ya msingi isuna, Ndugu Muro ameshangazwa na Namna fedha Takribani Milioni 17 zilivyotolewa Benki na Viongozi hao Bila Kuwashirikisha Wajumbe wa halmashauri ya kijiji na wajumbe wa kamati tatu za kusimamia mradi huo 


Kutokana na utata huo, Dc Muro amemuelekeza mkurugenzi wa halmashauri ya ikungi pamoja na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru kufuatilia mchakato mzima wa mradi huo ili kuondoa sintofahamu ya matumizi ya fedha na kuagiza ujenzi uendelee haraka uku uchunguzi ukifanyika.Share To:

Post A Comment: