Miradi yote ya maendeleo inatakiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa ili iweze kutoa huduma bora na mapema kwa wananchi.


Rai hiyo,imetolewa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 bwana Sahil Gararuma alipokuwa akikamilisha ukaguzi wa miradi mbalimbali katika halmashauri ya Meru.


Amesema miradi mingi katika halmashauri ya Meru ni mizuri hivyo juhudi kubwa iwekwe katika kuikamilisha kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma mapema.


Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya Meru umeweka jiwe la msingi miradi 2, kuzindua miradi 3 na kutembelea miradi 4 yenye thamani ya sh. bilioni 1.4.

Share To:

Post A Comment: