Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akitoa elimu kwa wananchi walofika kwenye Banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini hapa kunakoendelea maonyesho ya biashara kulia aliyekaa ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda

Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule za Msingi walofika kwenye Banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini hapa kunakoendelea maonyesho ya biashara  kulia aliyekaa ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda

Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga wakiwahudumia wananchi kama wasikiliza kwa umakini wananchi waliotembelea banda lao katika ni Mkaguzi wa NSSF Mkoa wa Tanga Hadija Mpungu kulia ni Afisa Mwandamizi wa NSSF Muheza Fatma Ally  kushoto ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda

Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama  katika akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Mkoa wa Tanga (TCCIA) Rashid Mwanyoka kushoto wakati walipotembelea banda lao
Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama   akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

 

NA OSCAR ASSENGA, TANGA. 

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) Mkoani Tanga umesema kwamba wanatumia  maonyesho ya Biashara ya mwaka 2022 yanayoendelea kwenye viwanja vya mwahako kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye mfuko huo

Hayo yalisemwa leo na Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya Biashara. 

Alisema kwamba uwepo wa maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka umekuwa na tija na kwa na bahati nzuri mwaka huu wao wamekuwa moja ya wadhamini hivyo wameona fursa nyingi zinatokea pamoja na kuwa na mkutano na wafanyabiashara na wao kuelezea changamoto walizokuwa nazo na nini kuboreshwe na nini kiongezwe kwenye huduma wanazotoa kwa mkoa huo.

"Kwa kweli niwaambie kwamba maonyesho ya mwaka huu  yamefana kuliko yalivyokuwa miaka iliyopita kutokana na washiriki wamekuwa wengi kutoka 62 mpaka 95 mwaka huu na hiyo ni faida kwetu kwani tumeweza kuandikisha wanachama 53 na waajiri wapya wawili"Alisema

Aliongeza kwamba hatua hiyo inawaweka vizuri katika malengo yao na inawasaidia kuongeza wanachama na kuongeza michango inayofikia kwenye malengo yao ya wanachama wa Sekta ya viwanda na Utalii ambapo kuna wajasiriamali wadogo kupitia NSSF sekta isiyokuwa rasmi wanaweza kuongea nao na kuweza kuwapa elimu na wawo kuweza kuwapa mapendekezo ya aina gani ya mafao watakayopenda .

Hata hivyo alisema tokea kuanza mwa maonyesho hayo mpaka sasa wamekwisha kuandikisha wanachama 51 na waajiri 3 huku lengo lao la siku 10 za maonyesho hayo waandikishe wanachama wapya 230 na waajiri 14.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: