Na,Jusline Marco;Simanjiro


Wafanyabiashara Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamepatiwa elimu juu ya matumizi sahihi ya mifuko mbadala na vifungashio vilivyokidhi vigezo na vilivyopitishwa na serikali kwa matumizi.


Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Kaskazini, Francis Nyamuhanga ameeataka wafanyabiashara hao kutumia vifungashik na mifuko mbadala kliyopitishwa na serikali ili kuweza kuzuia uchafuzi wa mazingira.


Amesema lengo kuu ni kutoa elimu hiyo kwa wananchi ni ufuatiliaji na uelimishaji  wa katazo la matumizi ya mifuko mbadala na vifungashio vya plastiki visivyokidhi viwango baada ya serikali kupiha marufuku mifuko ya plastiki na kuleta mifuko mbadala.


Aidha Nyamuhanga amesema matumizi ya mifuko mbadala na vifungashio ambavyo havijakidhi vigezo vya ubora na kuthibitishwa na serikali kunachangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la uchafuzi wa mazingira kutokana na vifungashio hivyo ah mifuko hiyo kutooza kwa haraka katika ardhi.


"Baada ya serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki mwaka 2019 na kuleta mifuko mbadala,bado kumekuwa  na mifuko mbadala isiyokidhi viwanho,kwahiyo tunatoa kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Mererani hapa Simanjiro kwenye masoko,kwenye maduka ya rejareja na ya jumla hata kwa wananchi kuwaelimisha kwamba mifuko mbadala inatakiwa iwe na viwango gani."alisema Francis Nyamuhanga Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Kaskazini


Afisa huyo ameainisha nembo zinapaswa kuonekana katika mifuko iliyokidhi vigezo vya ubora kuwa ni GSM 70,uwe na nembo ya kurejerezwa ambayo inatoa urahisi kwa mfuko kuweza kurudi kiwandani baada ya matumizi na kutengenezwa bidhaa nyingine,anuwani ya mzalishaji au nembo ya biashara inayoonyesha jina la kampuni iliyozalisha kifungashio hicho.


Vilevile ameongeza kuwa mfuko mbadala na kifungashio kilichokidhi ubora pia kinapaswa kuonyesha uwezo wa kubeba kwa maana ya kilogramu,iwe imethibitishwa ubora wake na shirika la viwango Tanzania TBS.


"Lakini baada ya kushughulika na mifuko mbadala kitu cha pili ni vifungashio ambavyo vinatakiwa pia viwe na anuwani ya mzalishaji,lakini pia ziwe na alama ya urejerezaji pamoja na unene usiopungua GSM 30 sambamba alama ya ubora inayotolewa na TBS."aliongeza Afisa huyo wa Mazingira NEMC Kanda ya Kaskazini


Sambamba na hayo Saimon Urassa Afisa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro katika zoezi hilo amesema kama serikali wamejitajidi kutoa elimu kwa wananchi juu matumizi ya mifuko iliyopigwa marufuku na serikali na kuweza kutumia mifuko na vifungashio ambavyo vimepitishwa na serikali kutumika.


"Nalishukuru Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC lwa kuona umuhimu wa kuja kutoa elimu zaidi na kuihamasisha jamii kuhusiana na makatazo ya mifuko hii."Alisema Saimon Urassa Afisa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: