Na Joel Maduka.


Wafanyabiashara wakubwa na makampuni wametakiwa kujitokeza kushiriki maonesho ya Fahari ya Geita yanayotarajia kuanza Tar 20 hadi 29 May 2022, ambayo lengo lake ni kutangaza fursa mbali mbali zilizopo Mkoani Geita zikiwemo za kilimo pamoja na ufugaji.


Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo kwenye ofisi za African creative zilizopo mtaa  Buhala hala,Mwenyekiti wa maandalizi ya Fahari ya Geita, Raphael Siyantemi amesema maonesho hayo yanatarajia kuwakutanisha wafanyabiashara wa ndani ya Mkoa na nje ya Nchi.


"Nimaonesho haya ni awamu ya tatu sasa lakini tumeona mwitikio umekuwa ni mkubwa kwa kipindi cha nyuma na sasa tunataka kuwaonesha watu juu ya Fahari ya Geita na fursa zilizopo ndani ya Mkoa wetu wa Geita" Raphael Siyantemi Mwenyekiti wa maandalizi ya Fahari ya Geita.


Kwa upande wake Katibu wa Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima,Mariam Mkaka amesema wanatarajia maonesho hayo kutumika kama sehemu ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji lakini pia kutangaza biashara zao pamoja na kubadilishana mawazo ya kibiashara.


"Sisi TCCIA ni washiriki wa maonesho ya Fahari ya Geita kwa maana tumejipanga kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji juu ya mbinu bora za kilimo lakini pia kuona namna ya kusaidia wakulima kutangaza shughuli zao"Mariam Mkaka mtendaji Mkuu wa TCCIA Geita.


Meneja wa SIDO Mkoani Geita, Jalfary Donge ametoa Wito kwa wafanyabiashara kutumia maonesho kama njia ya kujitangaza.


Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonesho hayo anatarajia kuwa Waziri wa viwanda na biashara Dr Ashatu Kijaji.


Share To:

JUSLINE

Post A Comment: