MKurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Ladislaus Matindi akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uwanja wa ndege wa Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa ziara hiyo

Meneja wa Uwanja wa Ndege Mkoani Tanga Mussa Mcholwa akizungumza wakati wa ziara hiyo

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Ladislaus Matindi katika akitembelea uwanja huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima na kushoto ni Meneja wa uwanja wa Ndege Tanga
Mussa Mcholwa
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima kulia akimuonyesha kitu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Ladislaus Matindi wakati wa ziara yake


NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

 

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) limesema lipo tayari kuanzisha safari zake za Tanga mara baada ya mpango wa upanuzi wa uwanja wa Ndege Tanza utakapokamilika

 

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Ladislaus Matindi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uwanja wa ndege wa Tanga ambapo alisema mkoa huo ni moja ya sehemu ambayo wamekuwa wakihudumia kwa miaka iliyopita.

 

Alisema lakini teknolojia ya viwanja na matakwa kubadilika hivyo kwa ndege waliyonayo hivi sasa ya kiwanja kuwa kifupi hakiwezi kuhimili uwezo wa ndege walizonazo. 

 

Aidha alisema upanuzi wa uwanja huo utahusisha njia ya kurukia ndege( runway)ili uweze kuwa na uwezo wa kuhudumia ndege na sababu ipo kubwa tuu kwa kuwa mzunguko hasa wa kibiashara Tanga ni mkubwa hivyo suala hilo serikali imeliona na kuanza kulifanyia kazi.

 

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Meneja wa Uwanja wa Ndege Mkoani Tanga Mussa Mcholwa alisema upanuzi huo wa uwanja utakapokamilika utasaidia kuongeza fursa za kibiashara na kiuchumi. 

 

"Ndege kubwa saizi ya kati zitatua mzunguko utaongezeka, sababu kama bombadier Q4100 inabeba abiria 80 kwahiyo mnaweza mkaona kutoka abiria 12 kwenye caravan mpaka abiria 80 hivyo sisi kama Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania tutaongeza, mapato pindi kiwanja hichi kitakapopanuliwa alibainisha," Meneja huyo. 

 

Aidha alisema kwamba Serikali inaangalia mpango wa namna ya upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mkoani Tanga ili kukiwezesha kuweza kuwa na  uwezo wa kutumiwa na ndege kubwa za abiria. 

 

Hata hivyo alisema mpango wa Serikali ni kukifanyia upanua kiwanja hicho kutoka mita 1250 zilizopo hivi sasa hadi kufikia mita 1700 ambazo zitawezesha ndege kubwa kuweza kutua. 

 

 

Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema Serikali inaangalia namna ya kuupanua uwanja huo ili uweze kuhudumia ndege  kubwa kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

 

Malima alisemaTanga ni moja ya mikoa ya  kibiashara hususani kwa wasafiri wa ndege kwani wapo watu wanaotamani kutoka Tanga kwenda kufanya shughuli zake maeneo mengine na jioni kurejea. 

 

 

Mwisho.


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: