Uhaba na uchafu wa vyoo wahatarisha Afya ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kizumbi, iliyopo Kata ya Kizumbi, Wilayani Shinyanga mjini.
Imedhibitika kwamba Wanafunzi 267, wa Shule hiyo wapo katika hatari ya kuugua magonjwa ya tumbo, yakiwamo yakuharisha kutokana na kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vyoo, hali inayowalazimu baadhi yao kujisaidia ovyo vichakani.
Hali hiyo imetokea baada ya choo walicho kuwa wanatumia kutitia na kuanguka hali hiyo imepelekea kutumia vyoo chakavu ambavyo sio salama kwa mazingira ya ndani ya choo hicho sio salama, kwa matumizi ya huduma hiyo.
Wakiongea na wanahabari Wanafunzi wa Shule hiyo walilalamika kuwa hali ya ukosefu wa vyoo, inapelekea wao kuchelewa vipindi kutokana na foleni vyooni na wakati mwingine wanalazimika kujisaidia haja kubwa na ndogo vichakani, kitu ambacho ni vigumu wao kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya kizumbi Ruben Kitinya, amesikitishwa na kitendo cha viongozi kulikalia kimya swala hilo wakati wanalijua na wamefika shuleni hapo na kujionea hali halisi ilivyoo.
Ameendelea kwa kusema kuwa Mkuu wa wilaya na Mbunge walisha fika na kuahidi kutengeneza lakini mpaka sasa ni miezi kadhaa imepita hakuna kilicho fanyika, alisema Ruben.
"Wanafunzi wanajisaidia hata kwenye vichaka kitu ambacho kinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko, nilisha toa taarifa kwa viongozi lakini hawajalichukulia katika hali ya dharula, naomba Halmashauri pamoja na Serikali kulichukulia ni jambo la dharula kuwanusuru watoto wetu", alisema Ruben.
Mjumbe mmoja ambaye ni mjumbe katika kamati ya shule hiyo, alieleza kuwa mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia katika shule ni kichocheo kwa mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao na kupata maarifa na ujuzi yatakayo wasaidia katika maisha yao.
" Muda mwingi tunawaona wanafunzi wakizurula mitaani na kuomba kutumia vyoo vya watu waliojenga karibu na shule, kitu ambacho wanatumia muda mwingi katika kutafuta sehemu ya kujistili, kuliko muda wa kukaa darasani" alisema mjembe huo ambaye hakutaka jina lake kitajwa.
Utafiti wetu pia umebaini kuwepo kwa shule nyingi za msingi na sekondari ambazo hazina Mazingira rafiki kwa wanafunzi, ikiwepo mifumo mizuri ya maji safi na taka, vyoo na vifaa vya usafi na sehemu ya kuhifazia tauro za wasichana.
Shule hiyo inajumla ya Wanafunzi 622, ambao hutumia matundu manne tu, hiyo inamaana Wanafunzi 84 hutumia tundu moja la choo.
Kwa mujibu wa Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2009, inaelekeza wasichana 20, watumie tundu moja la choo na wavulana 25, watumie tundu moja la choo.
Shule ya Kizumbi Sekondari inajumla ya wasichana 355, ambao hutumia matundu manne , na hili idadi hiyo ya wasichana ikidhi uwiano wa 1:20 inatakiwa wasichana hao wapate matundu ya 17, ambayo kwa sasa wanamatundu manne.
Kwa muktadha huo wanahitaji matundu kumi na tatu kukidhi mahitaji yote ya vyoo.
Idadi wavulana wa shule hiyo, wapo jumla 267, ambao ndio wahanga wakubwa wa changamoto ya kutokuwa na choo, na hivyo kuwalazimu kutumia vyoo chakavu vilivyokuwa vinatumika na wasichana miaka kadhaa nyuma, ambavyo navyo kiafya sio salama, nakuwalazimu kujisaidia vichakani.
Kulingana na Sera ya elimu kwa upande wa wavulana tu katika shule hiyo wanapaswa kuwa na matundu ya vyoo kumi na tatu, ili kukidhi kukizi mahitaji yote ya wavulana shuleni hapo.
Kwa ujumla shule hiyo inamapungu ya makubwa ya vyoo vya wanawake na inakabiliwa na changamoto ya kukosa vyoo vya wanaume na ni hatari zaidi, pale Wanafunzi wanapo jisaidia vichakani, hali iliyotufanya kufika shuleni hapo kujionea hali halisi ilivyo shuleni hapo.
Imeripotiwa kuwa Mara kadhaa viongozi wamekuwa wakifika shuleni hapo na kuahidi kulipatia ufumbuzi na pindi wanapoondoka inabaki kama simulizi za Bunawazi, alisema mjumbe mmoja wa kamati ya shule.
Kukosekana kwa vyoo vya wavulana katika Sekondari hiyo inaweza kuakisi hali halisi iliyopo katika shule mbalimbali Mkoani humo, ambapo kuna shule zingine hazina vyoo kabisa, na vipo ambazo zinavyoo vichache ambavyo havikidhi mahitaji ya Wanafunzi na kwenda kinyume na maelekezo ya Sera, na kuhatarisha afya za Wanafunzi hasa wa kike ambao hupata hedhi kila mwezi.
Licha ya kutokuwepo kwa vyoo vya wavulana katika shule hiyo lakini walimu bado wanalazimika kuwa funsisha Wanafunzi namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko na kuhakikisha afya za Wanafunzi zinapewa kipaumbele.
Timu ya wanahabari ilitaka ufafanuzi kutoka kwa Mkuu wa Mkoaa, Ofisini kwake hakuwepo, tulipompigia simu iliita pasipo kupokelewa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Jasinta Mboneko, alipokea ila alitutaka kwenda kwa afisa elimuSekondari, ili atupatie ufafanuzi kuhusu changamoto hiyo, kwa kuwa yeye hayupo ofisini amepatwa na msiba.
Tulipo mpigia afisa elimu Sekondari naye simu iliita pasipo kupokelewa.
Post A Comment: