Wateja Kupata GB 66 za intaneti bila malipo kwa mwaka mzima.

Dar es Salaam. Tarehe 22 Aprili, 2022. Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za  kidijitali nchini, Tigo Tanzania, imeshirikiana na Vivo Mobile Tanzania kuzindua simu ya kisasa ya Vivo Y01 inayotarajiwa kuuzwa kwa shilingi 250,000. 

Mteja yeyote atakayenunua Vivo Y01 kutoka kwa maduka ya Tigo au maduka ya Vivo kote nchini atapewa kifurushi cha ukaribisho bure kutoka Tigo ambacho kina GB 66 za Intaneti bila malipo kwa mwaka mzima.

Mtaalamu wa bidhaa za Intaneti kutoka Tigo, Blass Abdon akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema, “Tunafuraha kushirikiana na Vivo Mobile Tanzania kutambulisha simu ya kisasa ya Vivo Y01, ambayo itaongeza kasi ya ujumuishaji wa kidijitali nchini. Simu hiyo inapatikana kwa wote maduka ya Tigo kote nchini kuanzia leo.”

"Tuko thabiti katika azma yetu ya kuongeza kasi ya kupenya kwa simu janja za mkononi nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wanafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, tunatoa data ya intaneti ya GB 66 BURE kwa mwaka mzima. kwa wateja wote wanaonunua simu mahiri ya Vivo Y01.” Alisema Abdon.


"Vivo Y01 hakika inabadilisha ushindani katika soko la simu janja, inazidi kushika kasi na hakika haipungui. Tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa tunawaweka wateja wetu katika mstari wa mbele katika mawasiliano nchini Tanzania. Tumejitolea kukuweka mbele kwa kukupa teknolojia za hivi punde pamoja na miundo inayotegemeka na bora zaidi. Alisema Mtaalamu wa Mawasiliano wa Vivo Y01,Shadya Amiry.

Vivo YO1 ni Simu janja nyembamba na nyepesi ikilinganishwa na simu janja zingine za hali ya juu kwa bei sawa, simu yetu ina sifa tatu muhimu zifuatazo: -

• Betri kubwa (5000 mAh) yenye uwezo wa juu wa kuweka chaji kwa zaidi ya siku 2

. Saizi kubwa ya skrini ya inchi 6.51 ili kuvinjari mwonekano mzuri  zaidi


• Uwezo mkubwa wa kuhifadhi wa 32 gb. 

Alimalizia Mtaalam kutoka VIVO.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: