Na, Mwandishi Maalum,TMDA Kusini 


Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kusini kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imeteketeza dawa na vifaa tiba ambazo zimekwisha muda wa matumizi zenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na tano.

Kazi hii imefanyika katika hospitali ya Wilaya ya Liwale chini ya usimamizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri kupitia idara ya Afya baada ya kupata kibali kutoka kwa mhakiki mali wa Serikali.

Uteketezaji wa dawa na vifaa tiba hufanyika kwa kumfuata taratiba za Serikali na utunzaji wa mazingira basi wakati wa kufanya utekezaji kuna kuwepo ushirikishwaji wa idara ya mazingira, polisi na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba.




Share To:

JUSLINE

Post A Comment: