Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Samuel  Matura (kulia) akimuonesha ramani Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikungi mkoani Singida  ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Jerry Muro (kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo, walipokuwa wakikagua Msitu wa Asili wa Minyughe ambao umevamiwa na kufanyika uharibifu mkubwa wa mazingira.

Wajumbe wa kamati hiyo wakipitia ramani ya msitu huo.
Majadiliano yakifanyika wakati wa ziara hiyo.
Safari ya ukaguzi wa msitu huo ikifanyika.
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya msitu huo.
Muonekano wa mazao yaliyolimwa ndani ya msitu huo.
Muonekano sehemu ya msitu huo.
Magari yakichanja mbugu ndani ya msitu huo wakati wa ukaguzi.
Mashamba ya alizeti yakiwa yamelimwa ndani ya msitu huo.
Makazi ya kudumu ya watu yaliopo eneo la Njiapanda yakiwa ndani ya msitu huo.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akiwa mbele ya darasa la Shule Shikizi ya Ilowoko wakati wa ukaguzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkenene, Temael Kaali wakati wa ziara hiyo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


KAMATI ya Ulinzi na Usalama wilayani Ikungi ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wlaya hiyo Jerry Muro imetembelea na kukagua  Msitu wa Asili wa Minyughe ili kujionea changamoto mbalimbali zinazotishia kutoweka kwa msitu huo.

Katika ziara hiyo  kamati hiyo ilitembelea taasisi za Serikali zilizojengwa katika msitu huo hasa shule na kujionea tishio kubwa la kutoweka  kwa msitu huo kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama kilimo, ufugaji, ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na kuanzisha makazi.

Shule walizozitembelea ni Shule ya Msingi Mkenene,Shule Shikizi ya  Ilowoko, Shule Shikizi ya Munyu na Maghwagana ambapo pia katika maeneo hayo kuna makazi ya watu ya kudumu yalioanzishwa.

Akizungumza katika ziara hiyo iliyofanyika juzi ikiwahusisha viongozi waandamizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani humo, mkuu wa wilaya hiyo, Jerry Muro alisema lengo  la ziara hiyo ni kujiridhisha kabla ya hatua ya kuukabidhi msitu huo kwa TFS ambao wanauwezo mkubwa wa kuusimamia kutokana na umuhimu wake.

Alisema ziara ya namna hiyo ni ya nne na kuwa sasa wapo kwenye hatua ya mwisho ya kutumia busara na hekima ya namna gani wanaweza kuielimisha jamii iliyopo ndani ya msitu huo na kuzungumza nayo na wale waliopo mbembezo ili kwa pamoja waone ni njia gani ya maisha ifanyike ya kuendelea kuwepo ndani ya msitu huo bila ya kuuathiri  na msitu kuwepo bila ya kuathiri maisha ya wananchi.

"Hiki ndicho tunacho kifanya leo na ni lazima tujiridhishe na kuona hali ikoje na sisi kama Serikali tunaweza kufanya nini kunusuru msitu huu wa Minyughe na nyinyi mmeona wapo watu wanalima, wanakata miti,  wanafanya shughuli za kijamii hivyo ni lazima kuhifadhi msitu" alisema Muro.

Akitolea mfano wa majengo ya taasisi za Serikali alisema kuna Shule Shikizi ya Ilowoko ambayo zamani ilikuwa na madarasa mawili lakini baada ya kupata fedha Sh.Bioni 2.6 ndipo walipojenga madarasa manne na ofisi mbili za walimu hivyo kuboresha maisha ya wanafunzi na kuongeza thamani ya maisha ambapo kutoka makuu ya wilaya hadi kufika katika shule hiyo ni takribani kilometa 120 lakini wao hawakuangalia umbali bali kuboresha shule ambazo ziko pembezoni kabisa ya wilaya hiyo lakini changamoto kubwa ikiwa ni shule hiyo ipo ndani ya hifadhi ya msitu.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: