Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI ya Austria kupitia shirika la Sister Cities Salzburg –Singida
(SCSS) lililoko Salzburg Austria kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la Kiserikali la Community
Initiatives Promotion (CIP) la mkoani Singida limeendelea kuunga mkono jitihada
za Rais Samia Suluhu Hassan za kuinua
sekta ya elimu ambapo limewezesha kugharamia mafunzo ya lugha ya alama kwa
wazazi na walezi wenye watoto wenye usikivu hafifu (viziwi) wanaosoma Shule ya Msingi Tumaini Viziwi
iliyopo Manispaa ya Singida.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji
wa shirika la CIP , Afesso Ogenga alisema
walianza kuisaidia shule hiyo tangu mwaka 2005 hadi
sasa na kuwa
wamekuwa wakipewa ushirikiano mkubwa na Serikali mkoani hapa.
Alisema tangu mwaka huo wameweza kuisaidia shule
hiyo kwa kujenga madarasa mawili ofisi kuu ya zamani na vyoo vya mwanzo vya
wanafunzi,jiko, Bwalo na samani zake, Magodoro ya wanafunzi 66, Matundu manne
ya vyoo na chumba maalum cha wasichana na taulo zao (sodo) kwa mwaka mzima.
Alitaja msaada mwingine
waliotoa ni sare kaptula,sketi, shati, sweta na viatu kwa wanafunzi 20 wenye mazingira magumu, vifaa vya
kufundishia na kujifunzia (kamusi za Kiswahili 10, atlasi 10, kamusi ya English
Kiswahili mbili, chaki na rimu.
Alisema pia walitoa
msaada wa Photocopy machine, luninga na dishi la azam , mipira kwa michezo
yote, mafunzo ya lugha ya alama ambapo
mafunzo haya yaliyofikia tamati jana ni ya awamu ya tatu, ziara ya mafunzo
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwa wanafunzi wote na walimu na kulipia ada na
stationary kwa walimu wanaojiendeleza.
Ogenga
alisema matarajio yao kama mambo yatakwenda vizuri ni kutoa msaada mwingine kwa kutengeneza vitanda 25
(double deker), kufanya ziara ya kimasomo,kuwalipia
ada walimu wawili wanaojiendeleza, msaada kwa watoto 20 wenye mazingira magumu
kwa kuwanunulia sare za shule na kununua
vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Mwalimu Mkuu wa shule
hiyo, Francis Edward alisema wamekuwa
na mahusiano mazuri na shirika hilo tangu mwaka 2005 hadi sasa na limekuwa ni
sehemu ya shule kwani wamegusa maeneo mengi katika kuifanya ionekane kama
inavyoonekana.
.Akitoa historia fupi ya Shule
hiyo alisema ilianzishwa mwaka 2001 ikiwa na jumla ya wanafunzi watano kati yao
wavulana walikuwa wawili na wasichana watatu ambapo kwa sasa shule ina jumla ya
wanafunzi 84, wavulana 50 na wasichana 34, walimu nane wakiume watatu na wakike
watano na kuwa wanawalinzi, mpishi mmoja
na mwangalizi wa wanafunzi mmoja.
Alisema wazazi na walezi waliotunukiwa
vyeti baada ya kufuzu mafunzo hayo ni 39 na
walitoka Halmashauri zote za
wilaya Mkoa wa Singida, Manispaa na nje ya mkoa wa Singida.
Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa
hiyo, Tumaini Christopher alisema
wataendelea kushirikiana na mashirika hayo kwa ajili ya kusaidi watoto wa
makundi maalum na akawaomba wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa aina yoyote
wasiwafungie ndani na badala yake wawapeleke shuleni.
Baadhi ya miradi iliyotekelezwa na shirika hilo ni kukarabati madarasa mawili na ofisi ya walimu
katika Shule ya Msingi Ikhanoda iliyopo Halmashauri ya Wilaya Singida Vijijini
na katika mwaka wa fedha 2018-2019, SCSS
limetoa takribani sh. 135 milioni fedha za kitanzania kusaidia miradi ya
maendeleo katika Kata za Mwasauya na Ikhanoda zilizopo katika halmashauri hiyo. |
Post A Comment: