Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Siriel Mchembe amewataka wanawake ambao hawataki kuzaa watumie uzazi wa mpango kuliko kutupa watoto wachanga kuwa kitendo hicho ni zaidi ya unyama.


Mchembe amesema hayo wakati alipomtembelea mtoto aliyeokotwa siku 18 zilizopita wilayani humo ambapo anatunzwa na wauguzi wa hospitali ya mji Handeni kwenye kitengo cha watoto maalum, na kusema kuwa,hakuna sababu ya mwanamke kubeba mimba miezi tisa halafu anatupa mtoto.

Amesema kitendo hicho ni zaidi ya unyama kwani hata wanyama wenyewe hawawezi kufanya hivyo,ila baadhi ya wanawake bila kufikiria hatma ya kiumbe huyo ana amua kumtupa.

"Niwaombe sana wanawake wenzangu Mungu ametupa roho nzuri kama hutaki kuzaa tumia uzazi wa mpango kutupa mtoto ni zaidi ya unyama,maana hata wanyama wenyewe hawawezi kufanya kitendo hiki kibaya,kwanza inawezekana mtoto ni huyo huyo na unaweza usipate mwingine",amesema Mchembe.

Pia Mchembe amewaomba wadau kuangalia uwezekano wa kuanzisha kituo cha kulelea watoto yatima,kwani Handeni imekuwa na inahitajika huduma kama hiyo.

Mganga mkuu halmashauri ya mji Handeni Feisal Said akizungumzia hali ya mtoto huyo amesema,anaendelea vizuri baada ya vipimo  na hakuwa na tatizo lolote la kiafya na wanaendelea kumpa huduma.

Ameongeza kuwa wamemfanyia vipimo mbalimbali na afya ya mtoto ni nzuri,hatua ilibakia kwasasa ni kusafirishwa kupelekwa kituo cha kulelea watoto yatima Lushoto.

Muuguzi Saida Zombe ambae alikuwa akimhudumia mtoto huyo ameeleza kwa uchungu hali ambayo alikuwa nayo mtoto baada ya kuokotwa kuwa hali ilikuwa ni mbaya kwani alikutwa na michubuko mwili.

"Siku aliyokuja alikuwa anasikitisha sana alikuwa anatoa harufu na makovu mwilini,ila kwasasa baada ya kumhudumia anaendelea vizuri sasa ana kilo 3.7 na amechangamka vizuri kama watoto wengine",amesema Saida.

Hata hivyo baada ya ombi la mkuu wa wilaya kuomba wadau kuangalia uwezekano wa kuanzishwa kituo cha kulelea watoto yatima,Mkurugenzi Mwandamizi Shirika la World Vision Tanzania Dokta Joseph Mayala amesema wataangalia suala hilo.

Amesema shirika la World Vision Tanzania lipo kwaajili ya kuhudumia watoto zaidi,hivyo wataangalia uwezekano wa kuweza kufanya utaratibu wa kusaidia kuwepo kituo cha watoto yatima na jina lake kinaweza kuitwa Gift.

Mtoto huyo ni watatu mpaka sasa kuokotwa wilayani Handeni ambapo wengine wawili waliokotwa kwa nyakati tofauti.

Imeelezwa kuwa kila kunapokucha hasa kwenye nchi za bara Afrika kunaripotiwa visa vya kutupwa kwa watoto wachanga mara wazaliwapo.

Na ukatili huo hufanywa mara nyingi na wazazi ambao ama hawana mipango ya kuchukua majukumu ya kuwalea watoto hao au kutokana na sababu moja au nyingine, huku wengi wakiokotwa barabarani , kwenye majaa ya taka na wengine wakiwa wametelekezwa kwenye mahospitali.

Aidha serikali kupitia Program Jumuishi ya Malezin,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto PJT-MMMAM 2021/22-2025/26 inasema Malezin Kwa Makuzi na Maendeleo ya mtoto (CCD)  ni mkoba ulioandaliwa wenye mbinu zilizoyhibitishwa  na shirika ya Afya Duniani  WHO na Shirika  la Kimataifa la kuhufumia  watoto UNICEF kwaajili ya watoa huduma  za afya  ili kutoa unasihi kwenye michezo  na mawasiliano  Kwa Wazazi / walezi wenye watoto wenye umri wa miaka 0-3 wakati  wa utoaji  huduma za afya.

Hata hivyo serikali Kwa kushirikiana  na wadau wa Maendeleo kupitia WAMJM  kitengo Cha afya ya Mama na Mtoto imeanza kuwekeza kwenye Malezin yenye mwitikio  Kwa kujumuosha  mbinu za Malezi Kwa Makuzi  na Maendeleo  ya mtoto pamoja na mafunzo ya ufuatiliaji wa ukuaji wa Maendeleo  ya mtoto.

Share To:

Post A Comment: