Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameahidi kusaidia uchimbaji wa visima kwenye misikiti kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ambayo hayana mtandao wa maji.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo leo,kuitikia ombi la uchimbaji wa visima kwenye misikiti ya pembezoni ya Jijini Dodoma,wakati wa hafla ya kutoa mkono wa futari kwa walimu wa madrasa na viongozi wa dini Jijini Dodoma hafla iliyofanyika kwenye Msikiti wa Gadafi Dodoma.
“Nina furaha kubwa sana kukutana nanyi tena siku ya leo katika mwezi huu wa mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni desturi yetu ya kukutana na kupeana mkono wa kheri kwa mwezi huu mtukufu.
Nimesikia ombi lenu la visima vya maji,nataka niwahakikishie kwamba ombi lenu la visima nimelipokea na nitalifanyia kazi kwa kutafuta wadau mbalimbali na Taasisi za Dini ya Kiislamu ambao tumekuwa tukishirikiana nao katika uchimbaji wa visima vya maji”Alisema Mavunde
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Dini wa Jijini Dodoma,Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shaban amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kujitoa kwa ajili ya shughuli za
Kijamii na hasa zinazogusa waislamu wa Dodoma na kutumia fursa hiyo pia kuwaomba viongozi hao kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wote ili kulisimamia Taifa hili katika misingi ya umoja na mshikamano.
Post A Comment: