Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe. Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki. Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taifa la Tanzania ni kusimama katika haki. Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na za kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipaswav
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: